Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mithali - Mithali 12

Mithali 12:2-27

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2Yehova humpa fadhila mtu mwema, bali mtu ambaye hufanya mipango ya ufisada atahukumiwa.
3Mtu hawezi kuimarishwa kwa uovu, bali wale watendao haki hawawezi kung'olewa.
4Mke mwema ni taji ya mume wake, bali yule aletaye aibu ni kama ugonjwa unaoozesha mifupa yake.
5Mipango ya wale watendao haki ni adili, bali shauri la mwovu ni udanganyifu.
6Maneno ya watu waovu ni uviziaji unaosubiri nafasi ya kuua, bali maneno ya mwenye haki yatawatunza salama.
7Watu waovu wametupwa na kuondolewa, bali nyumba ya wale watendao haki itasimama.
8Mtu husifiwa kwa kadri ya hekima yake, bali yule anayechagua ukaidi hudharauliwa.
9Bora kuwa na cheo duni- kuwa mtumishi tu- kuliko kujisifu kuhusu ukuu wako bila kuwa na chakula.
10Yule atendaye haki anajali mahitaji ya mnyama wake, bali huruma ya mwovu ni ukatili.
11Yule atendaye kazi katika shamba lake atapata chakula tele, bali anayesaka miradi duni hana akili.
12Watu waovu hutamani wanavyoiba watu wabaya kutoka kwa wengine, bali tunda la wale watendao haki hutoka kwao mwenyewe.
13Mtu mbaya hunaswa kwa maongezi yake mabaya, bali wale watendao haki hujinasua katika taabu.
14Mtu hushiba vitu vyema kutokana na tunda la maneno yake, kama vile kazi ya mikono yake inavyompa thawabu.
15Njia ya mpumbavu ni sawa machoni pake mwenyewe, bali mtu wa hekima husikiliza ushauri.
16Mpumbavu huonyesha hasira yake papo hapo, bali asiyejali tusi ni mwenye busara.
17Asemaye ukweli huongea ilivyo haki, bali shahidi wa uongo huongea uongo.
18Maneno yake asemaye kwa pupa ni kama kurusha upanga, bali ulimi wa mwenye hekima huleta uponyaji.
19Midomo yenye kweli itadumu milele, bali ulimi wa uongo ni kwa kitambo kidogo tu.
20Kuna udanganyifu katika mioyo ya wale wanaopanga kutenda uovu, bali furaha hutoka kwa washauri wa amani.
21Hakuna ugonjwa utakaowajia wale watendao haki, bali watu waovu watajazwa matatizo.
22Yehova anachukia midomo ya uongo, bali wale ambao huishi kwa uaminifu ndiyo furaha yake.
23Mtu mwenye busara anasitiri maarifa yake, bali moyo wa wapumbavu hupiga yowe za kipumbavu.
24Mkono wa mwenye bidii utatawala, bali watu wavivu watawekwa katika kazi za kulazimishwa.
25Mashaka katika moyo wa mtu humwelemea, bali neno zuri humfurahisha.
26Mwenye haki ni kiongozi kwa rafiki yake, bali njia ya waovu huwaongoza katika kupotea.
27Watu wavivu hawawezi kubanika mawindo yao wenyewe, bali mtu wenye bidii atapata mali zenye thamani.

Read Mithali 12Mithali 12
Compare Mithali 12:2-27Mithali 12:2-27