Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mhubiri - Mhubiri 9

Mhubiri 9:7-18

Help us?
Click on verse(s) to share them!
7Nenda zako, kula mkate wako kwa furaha, na kunywa mvinyo wako na moyo wa furaha, kwa kuwa Mungu huruhusu kusherehekea kazi njema.
8Nguo zako ziwe nyeupe siku zote, na kichwa chako kipake mafuta.
9Ishi kwa furaha na mwanamke umpendaye siku zako zote za maisha yako ya ubatili, siku ambazo Mungu amekupatia chini ya jua wakati wa siku zako za ubatili. Hiyo ni thawabu kwa ajili ya kazi yako chini ya jua.
10Chochote mkono wako unakifanya, kifanye kwa nguvu zako kwa sababu hakuna kazi, au ufafanuzi au ujuzi au hekima katika Sheol, unapoenda.
11Nimeona baadhi ya vitu vyakuvutia chini ya jua: Mashindano hayatokani na watu wenye mbio. Vita havitokani na watu imara. Mkate hautokani na watu wenye busara. Mali hazitokani na watu wenye ufahamu. Kibali hakitokani na watu wenye ujuzi. Badala yake muda na bahati huwaathiri wao wote.
12Kwa kuwa hakuna anaye fahamu wakati wake wa kufa, kama vile samaki wanaswavyo katika nyavu ya kifo, au kama vile ndege akamatwavyo katika mtego. Kama wanyama wanadamu wamefungwa katika nyakati mbaya ambazo ghafla huwaangukia.
13Pia nimeona hekima chini ya jua kwa namna ambayo kwangu ilionekana kubwa.
14Kulikuwa na mji mdogo na watu wachache ndani yake, na mfalme mkuu akaja kinyume na mji huo na akauzingira na akajenga mahandaki kwa ajili ya kuushambulia.
15Na katika mji kulikuwa na masikini, mtu mwenye hekima, ambaye kwa hekima yake aliuokoa mji. Ila baadaye aliye mkumbuka yule masikini.
16Hivyo, nikasema, “Hekima ni bora kuliko nguvu, lakini hekima ya mtu masikini hudharauliwa, na maneno yake hayasikilizwi.”
17Maneno ya watu wenye hekima yaliongewa polepole yanasikiwa vizuri kuliko makelele ya mtawala yeyote miongoni mwa wapumbavu.
18Hekima ni bora kuliko silaha za vita, lakini mwenye dhambi mmoja anaweza kuharibu mazuri mengi.

Read Mhubiri 9Mhubiri 9
Compare Mhubiri 9:7-18Mhubiri 9:7-18