Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mhubiri - Mhubiri 9

Mhubiri 9:3-12

Help us?
Click on verse(s) to share them!
3Kuna mwisho mwovu kwa kila kitu kinachofanyika chini ya jua, na mwisho kwa kila mtu. Moyo wa mwanadamu umejaa uovu, na wazimu uko katika mioyo yao wakati wanaishi. Hivyo baada ya hilo wanaenda kwa wafu.
4Kwa kuwa yeyote anayeungana na wote walio hai kuna tumaini, kama vile mbwa aliye hai ni bora kuliko simba aliye kufa.
5Kwa kuwa watu walio hai, lakini walio kufa hawajui chochote. Hawana tena tuzo yeyote kwa sababu kumbukumbu yao imesahaulika.
6Upendo wao, chuki na wivu vimekatiliwa mbali muda mwingi. Hawatapata sehemu katika kitu chochote kinachofanyika chini ya jua.
7Nenda zako, kula mkate wako kwa furaha, na kunywa mvinyo wako na moyo wa furaha, kwa kuwa Mungu huruhusu kusherehekea kazi njema.
8Nguo zako ziwe nyeupe siku zote, na kichwa chako kipake mafuta.
9Ishi kwa furaha na mwanamke umpendaye siku zako zote za maisha yako ya ubatili, siku ambazo Mungu amekupatia chini ya jua wakati wa siku zako za ubatili. Hiyo ni thawabu kwa ajili ya kazi yako chini ya jua.
10Chochote mkono wako unakifanya, kifanye kwa nguvu zako kwa sababu hakuna kazi, au ufafanuzi au ujuzi au hekima katika Sheol, unapoenda.
11Nimeona baadhi ya vitu vyakuvutia chini ya jua: Mashindano hayatokani na watu wenye mbio. Vita havitokani na watu imara. Mkate hautokani na watu wenye busara. Mali hazitokani na watu wenye ufahamu. Kibali hakitokani na watu wenye ujuzi. Badala yake muda na bahati huwaathiri wao wote.
12Kwa kuwa hakuna anaye fahamu wakati wake wa kufa, kama vile samaki wanaswavyo katika nyavu ya kifo, au kama vile ndege akamatwavyo katika mtego. Kama wanyama wanadamu wamefungwa katika nyakati mbaya ambazo ghafla huwaangukia.

Read Mhubiri 9Mhubiri 9
Compare Mhubiri 9:3-12Mhubiri 9:3-12