Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mhubiri - Mhubiri 8

Mhubiri 8:2-11

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2Ninakushauri kuitii amri ya mfalme kwa sababu ya kiapo cha Mungu cha kumlinda yeye.
3Usiharakishe kuondoka mbele ya uwepo wake, na usisimame kuunga mkono jambo lisilofaa, kwa kuwa mfalme anafanya chochote anacho tamani.
4Neno la mfalme hutawala, kwa hiyo ni nani atakaye mwambia, 'Unafanya nini?
5Yeyote ashikaye amri za mfalme hukwepa madhara. Moyo wa mwenye hekima hutambua mwelekeo muafaka na muda wa kuenda.
6Kwa kuwa kila jambo lina jibu sahihi, na wakati wa kujibu, kwa sababu taabu ya mtu ni kubwa.
7Hakuna anaye fahamu kinacho fuata. Ni nani awezaye kumwambia nini kinacho kuja?
8Hakuna mwenye uwezo juu ya roho aizuie roho; wala hana mamlaka juu ya siku ya kufa; wala hakuna kuruhusiwa katika vita vile; wala uovu hautamwokoa yule aliyeuzoea.
9Mambo hayo yote nimeyaona, nikatia moyo wangu katika kila kazi iliyofanyika chini ya jua. Kuna wakati ambapo mtu mmoja anayo mamlaka juu ya mwenziwe kwa hasira yake.
10Hivyo niliwaona wabaya wakizikwa hadharani. Waliondolewa mahali patakatifu na kuzikwa mahali waliposifiwa na watu katika mji walipokuwa wamefanya matendo maovu. Hii nayo haifai.
11Wakati hukumu dhidi ya tendo ovu haihukumiwi haraka, hushawishi mioyo ya wanadamu kutenda ubaya.

Read Mhubiri 8Mhubiri 8
Compare Mhubiri 8:2-11Mhubiri 8:2-11