Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mhubiri - Mhubiri 6

Mhubiri 6:2-8

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2Mungu anaweza kumpa mtu mali na utajiri na heshima kwa kiasi kwamba hakosi chochote anachokitamani mwenyewe, lakini kisha hampi uwezo wa kukifurahia. Badala yake mtu mwingine hutumia vitu vyake. Huu ni mvuke, teso baya.
3Kama mtu akizaa watoto mia moja na kuishi miaka mingi, ili kwamba siku za miaka yake ni nyingi, lakini kama moyo wake hautosheki kwa mema na hazikwi kwa heshima, kisha ninasema kwamba, mtoto aliyezaliwa akiwa amekufa ni bora kuliko alivyo.
4Hata mtoto huyo amezaliwa bila faida na anapita katika giza, na jina lake linabaki limefichika.
5Ingawa mtoto huyu haoni jua au kujua kitu chochote, ana pumziko ingawa mtu huyo hakupumzika.
6Hata kama mtu akiishi miaka elfu mbili lakini hajifunzi kufuraia vitu vizuri, aenda sehemu moja kama mtu yeyote yule.
7Ingawa kazi yote ya mtu ni kujaza mdomo wake, ila hamu yake haishibi.
8Hakika ni faida gani aliyo nayo mwenye hekima kuliko mpumbavu? Ni faida gani aliyo nayo masikini hata kama anajua jinsi ya kutenda mbele ya watu?

Read Mhubiri 6Mhubiri 6
Compare Mhubiri 6:2-8Mhubiri 6:2-8