Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mhubiri - Mhubiri 5

Mhubiri 5:6-20

Help us?
Click on verse(s) to share them!
6Usiuruhusu mdomo wako kusababisha mwili wako kutenda dhambi. Usiseme kwa mtumwa wa kuhani, “Kile kiapo kilikuwa kwa makosa.” Kwani nini kumfanya Mungu akasirike kwa kuapa kwa uongo, kumchochea Mungu aharibu kazi ya mikono yako?
7Kwa kuwa katika ndoto nyingi, kama ilivyo katika maneno mengi, kuna mvuke ubatili. Hivyo mwogope Mungu.
8Unapomwona masikini akiteswa na kunyang'anywa haki na kutendewa vibaya katika jimbo lako, usishangae kama kwamba hakuna anaye fahamu, kwa sababu kuna watu katika mamlaka ambao hutazama, kuna hata walio juu yao.
9Kwa nyongeza uzalishaji wa ardhi ni kwa kila mmoja, na mfalme mwenyewe huchukua uzalishaji kutoka mashambani.
10Yeyote apendaye fedha hatatosheka na fedha, na yeyote apendaye utajiri mara zote hutaka zaidi. Huu pia ni mvuke.
11Kadri mafanikio yanapoongezeka, ndivyo wanavyoongezeka watu wanaotumia. Kuna faida gani katika utajiri kwa mmiliki isipokuwa kuutazama kwa macho yake?
12Usingizi wa mfanyakazi ni mtamu, kama anakula kidogo au sana, lakini utajiri wa mtu tajiri haumuruhusu yeye kulala vizuri.
13Kuna jambo baya zaidi ambalo nimeliona chini ya jua: mali iliyowekwa akiba na mwenye nayo, inamsababishia taabu mwenyewe.
14Wakati tajiri anapopoteza utajiri wake kwa bahati mbaya, mwana wake, ambaye amemzaa, habakiziwi chochote mikononi mwake.
15Kama mtu azaliwavyo uchi kutoka tumboni mwa mamaye, vivyo hivyo ataondoka katika maisha haya akiwa uchi. Hachukui chochote kutoka katika kazi yake.
16Jambo jingine baya kabisa, kama mtu alivyo kuja ni lazima aende vivyo hivyo. Hivyo ni faida gani mtu yeyote aipatayo katika kufanya kwa ajili ya upepo?
17Wakati wa siku zake anakula gizani na anafedheheshwa sana na magonjwa na hasira.
18Tazama, kile nilichokiona kuwa kizuri kufaaa ni kula na knywa na kufurahia faida kutoka katika kazi zetu zote, tuzifanyazo chini ya jua wakati wa siku za maisha haya ambayo Mungu ametupa. Kwa kuwa huu ni wajibu wa mtu.
19Yeyote ambaye Mungu amempa mali na utajiri na uwezo wa kupokea sehemu yake na kufurahi katika kazi yake hii ni zawadi kutoka kwa Mungu.
20Kwa kuwa mara kadhaa hakumbuki siku za maisha yake, kwa sababu Mungu anamfanya kuhangaika na mambo ambayo anafurahia kuyafanya.

Read Mhubiri 5Mhubiri 5
Compare Mhubiri 5:6-20Mhubiri 5:6-20