Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mhubiri - Mhubiri 5

Mhubiri 5:2-11

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2Usiwe mwepesi wa kuongea kwa mdomo wako, na usiufanye moyo wako kuleta jambo lolote kwa haraka mbele za Mungu. Mungu yuko mbinguni, lakini uko chini, kwa hiyo maneno yako yawe machache.
3Kama una mambo mengi ya kufanya na kuhangaika, pengine utapata ndoto mbaya. Na pengine utaongea maneno mengi ya upumbavu.
4Ukiweka nadhili kwa Mungu, usichelewe kuifanya, kwa kuwa Mungu hafurahii upumbavu. Fanya kile ulichoapa utakifanya.
5Ni bora kutokuweka nadhiri kuliko kuweka nadhiri ambayo usiyoiondoa.
6Usiuruhusu mdomo wako kusababisha mwili wako kutenda dhambi. Usiseme kwa mtumwa wa kuhani, “Kile kiapo kilikuwa kwa makosa.” Kwani nini kumfanya Mungu akasirike kwa kuapa kwa uongo, kumchochea Mungu aharibu kazi ya mikono yako?
7Kwa kuwa katika ndoto nyingi, kama ilivyo katika maneno mengi, kuna mvuke ubatili. Hivyo mwogope Mungu.
8Unapomwona masikini akiteswa na kunyang'anywa haki na kutendewa vibaya katika jimbo lako, usishangae kama kwamba hakuna anaye fahamu, kwa sababu kuna watu katika mamlaka ambao hutazama, kuna hata walio juu yao.
9Kwa nyongeza uzalishaji wa ardhi ni kwa kila mmoja, na mfalme mwenyewe huchukua uzalishaji kutoka mashambani.
10Yeyote apendaye fedha hatatosheka na fedha, na yeyote apendaye utajiri mara zote hutaka zaidi. Huu pia ni mvuke.
11Kadri mafanikio yanapoongezeka, ndivyo wanavyoongezeka watu wanaotumia. Kuna faida gani katika utajiri kwa mmiliki isipokuwa kuutazama kwa macho yake?

Read Mhubiri 5Mhubiri 5
Compare Mhubiri 5:2-11Mhubiri 5:2-11