Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mhubiri - Mhubiri 12

Mhubiri 12:5-13

Help us?
Click on verse(s) to share them!
5Utakuwa wakati ambapo watu wataogopa vilivyoinuka na hatari iliyoko barabarani, na wakati ambapo mlozi utachanua maua, na wakati panzi watakapokokotana wenyewe, na wakati ambapo hamu za asili zitakaposhindwa. Kisha mtu aenda katika nyumba yake ya milele na waombolezaji watelemka mitaani.
6Mkumbuke Muumba wako kabla ya kamba ya fedha kukatwa, au bakuli ya dhahabu kupasuka, au gudulia kuvunjwa kwenye chemuchemi, au torori la maji kuvunjika kisimani,
7kabla mavumbi kurudia mahali yalipotoka, na roho kurudi kwa Mungu aliyeitoa.
8Kama ukungu wa mvuke,” asema mwalimu, kila kitu ni mvuke upoteao.
9Mwalimu alikuwa na hekima na aliwafundisha watu maarifa. Alisoma na kuazimu na kutunga mithali nyingi katika mpangilio.
10Mwalimu alitafuta kuandika kwa kutumia vithibitisho dhahiri, maneno ya kweli yaliyo wima.
11Maneno ya watu wenye hekima ni kama mchokoo. Kama misumari ilivyogongomewa kwa undani, ndivyo yalivyo maneno ya mabwana katika mkusanyiko wa mithali zao, ambayo yamefundishwa na mchungaji mmoja.
12Mwanangu kuwa makini na kitu zaidi, utengezaji wa vitabu vingi, ambacho hakina mwisho, na kusoma kwingi huleta uchovu mwilini.
13Mwisho wa jambo baada ya kila kitu umesikika, ni kwamba ni lazima umche Mungu na kushika amri zake, kwa kuwa huu ndilo jukumu lote la mwanadamu.

Read Mhubiri 12Mhubiri 12
Compare Mhubiri 12:5-13Mhubiri 12:5-13