Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Matendo ya Mitume - Matendo ya Mitume 8

Matendo ya Mitume 8:27-39

Help us?
Click on verse(s) to share them!
27Akaangaza na kwenda. Tazama, kulikuwa na mtu wa Ethiopia, towashi mwenye mamlaka kuu chini ya kandase; malkia wa Ethiopia. Aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu.
28Alikuwa akirejea ameketi garini mwake akisoma chuo cha nabii Isaya.
29Roho akasema na Filipo, “Sogea karibu na gari hili ukashikamane nalo.
30“Hivyo Filipo akaenda mbio, akamsikia akisoma katika chuo cha nabii Isaya; akasema, Je unafahamu unachosoma?”
31Muethiopia akasema, “nitawezaje mtu asiponiongoza?” Akamsihi Filipo apande garini na kuketi pamoja naye.
32Sasa fungu la maandiko alilokuwa akisoma Muethiopia ni hili; Aliongozwa kama kondoo kwenda machinjioni kuchinjwa; na kama kondoo alinyamaza kimya, hakufungua kinywa chake:
33Kwa kuhuzunishwa kwake hukumu yake iliondolewa: Nani ataeleza kizazi chake? maisha yake yameondolewa katika nchi.”
34Hivyo towashi akamwuliza Filipo, na kusema, “nakuomba, ni nabii yupi ambaye anaongelewa habari zake, ni kuhusu yeye, au za mtu mwingine”?.
35Filipo alianza kuongea, alianza kwa andiko hili la Isaya kumhubiria habari za Yesu.
36Wakiwa njiani, wakafika penye maji,' towashi akasema, “Tazama, pana maji hapa nini kinazuia nisibatizwe?,
37maneno haya, “Hivyo Muethiopia akajibu “naamini kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu,” hayamo kwenyemaandiko ya kale). Ndipo Muethiopia akaamuru gari lisimame.
38Walikwenda ndani ya maji, pamoja Filipo na towashi, Filipo akambatiza.
39Wakati walipotoka kwenye maji, Roho wa Bwana ikampeleka Filipo mbali; towashi hakumwona, akaenda njia yake akishangilia.

Read Matendo ya Mitume 8Matendo ya Mitume 8
Compare Matendo ya Mitume 8:27-39Matendo ya Mitume 8:27-39