Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Matendo ya Mitume - Matendo ya Mitume 2

Matendo ya Mitume 2:2-21

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2Ghafla ikatokea muungurumo kutoka mbinguni kama upepo mkali. ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi.
3Hapo zikawatokea ndimi, kama ndimi za moto zimegawanyika, zikawa juu yao kila mmoja wao.
4Wao wote wakajazwa na Roho Mtakatifu na wakaanza kusema kwa lugha zingine, kama vile Roho alivyowajalia kusema.
5Sasa walikuwapo wayahudi waliokuwa wanaishi Yerusalemu, wacha Mungu, kutoka kila taifa chini ya mbingu.
6Ngurumo hizi ziliposikiwa, kundi la watu likaja pamoja na wakiwa na wasiwasi kwa sababu kila mtu aliwasikia wakiongea kwa lugha yake mwenyewe.
7waliduwaa na kushangazwa, wao walisema, “Kweli, hawa wote wanaoongea siyo Wagalilaya?
8Kwa nini sisi tunawasikia, kila mmoja katika lugha tulizozaliwa nazo?
9Waparthia na Wamedi na Waelamu, na hao waishio Mesopotamia, Uyahudi, na Kapadokia, na katika Ponto na Asia,
10katika Frigia, Pamfilia, katika Misri, na sehemu ya Libya hata Kirene, na wageni kutoka Rumi,
11Wayahudi na waongofu, Wakrete na Waarabu, tunawasikia wakizungumza katika lugha zetu kuhusu kazi za uweza wa Mungu.”
12Wote walikuwa wameduwaa na kutatanishwa; walisemezana wao kwa wao, “Hii ina maana gani?”
13Lakini wengine walidhihaki wakisema, “Hawa wamejazwa kwa mvinyo mpya.”
14Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti, akawaambia, “Watu wa Yudea na wote mnaoishi hapa Yerusalemu, hili lijulikane kwenu, sikilizeni kwa makini maneno yangu.
15Watu hawa hawajalewa kama mnavyodhani, sababu saa hizi ni asubuhi saa tatu.
16Lakini hili lilikuwa limesemwa kupitia kwa nabii Yoeli:
17Itakuwa katika siku za mwisho; Mungu asema, nitamwaga Roho wangu kwa watu wote. Wana wenu na binti zenu watatoa unabii, vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto.
18Vilevile juu ya watumishi wangu na watumishi wangu wa kike katika siku hizo, nitamwaga Roho wangu, nao watatabiri.
19Nitaonesha maajabu juu angani na ishara chini duniani, damu, moto, na mafusho ya moshi.
20Na jua litabadilishwa kuwa giza na mwezi kuwa damu, kabla haijaja siku kuu na ya ajabu ya Bwana.
21itakuwa ya kwamba kila mmoja ambaye huliitia jina la Bwana ataokoka.'

Read Matendo ya Mitume 2Matendo ya Mitume 2
Compare Matendo ya Mitume 2:2-21Matendo ya Mitume 2:2-21