Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Matendo ya Mitume - Matendo ya Mitume 27

Matendo ya Mitume 27:17-43

Help us?
Click on verse(s) to share them!
17Baada ya kuwa wameivuta, walitumia kamba kuifunga meli. Waliogopa kwamba tungeweza kwenda kwenye eneo la mchanga mwingi la Syiti, hivyo wakashusha nanga na waliendeshwa kandokando.
18Tulipigwa kwa nguvu sana na dhoruba, hivyo siku iliyofuata mabaharia wakaanza kutupa mizigo kutoka melini.
19Siku ya tatu, mabaharia wakaanza kuyatoa maji kwa mikono yao wenyewe.
20Wakati ambapo jua na nyota hazikutuangazia kwa siku nyingi, bado dhoruba kubwa ilitupiga, na matumaini kwamba tungeokolewa yalitoweka.
21Baada ya kuwa wameenda muda mrefu bila chakula, hapo Paulo akasimama katikati ya mabaharia akasema, “Wanaume, mlipaswa mnisikilize, na tusingengo'a nanga kutoka Krete, ili kupata haya madhara na hasara.
22Na sasa nawafariji mjitie moyo, kwa sababu hakutakuwa upotevu maisha kati yenu, isipokuwa hasara ya meli tu.
23Kwa sababu usiku uliopita malaika wa Mungu, ambaye huyo Mungu mimi ni wake, na ambaye ninamwabudu pia - malaika wake alisimama pembeni mwangu
24na kusema, “Usiogope Paulo. Lazima usimame mbele ya Kaisari, na tazama, Mungu katika wema wake amekupa hawa wote ambao wanasafiri pamoja nawe.
25Hivyo, wanaume, jipeni moyo, kwa sababu namwamini Mungu, kwamba itakuwa kama nilivyoambiwa.
26Lakini lazima tuumie kwa kupigwa katika baadhi ya visiwa.”
27Ulipofika usiku wa kumi na nne, tulipokuwa tukiendeshwa huko na huko kwenye bahari ya Adratik, kama usiku wa manane hivi, mabaharia walifikiri kwamba wamekaribia nchi kavu.
28Walitumia milio kupima kina cha maji na wakapata mita thelathini na sita, baada ya muda mfupi wakapima tena wakapata mita ishirini na saba.
29Waliogopa kwanza tunaweza kugonga miamba, hivyo wakashusha nanga nne kutoka katika sehemu ya kuwekea nanga na wakaomba kwamba asubuhi ingekuja mapema.
30Wale mabaharia walikuwa wanatafuta namna ya kuitelekeza ile meli na walizishusha majini boti ndogo ndogo za kuokolea maisha, na wakajifanya kwamba wanatupa nanga kutoka sehemu ya mbele ya boti.
31Lakini Paulo akamwambia yule askari wa jeshi la Kiroma na wale askari, “Hamuwezi kuokoka isipokuwa hawa watu wanabaki kwenye meli”.
32Kisha wale askari wakakata kamba za ile boti na ikaachwa ichukuliwe na maji.
33Wakati mwanga wa asubuhi ulipokuwa unajitokeza, Paulo akawasihi wote angalau wale kidogo. Akasema, “Hii ni siku ya kumi na nne mnasuburi bila kula, hamjala kitu.
34Hivyo nawasihi mchukue chakula kidogo, kwa sababu hii ni kwa ajili ya kuishi kwenu; na hakuna hata unywele mmoja wa vichwa vyenu utakaopotea.
35Alipokwisha kusema hayo, akachukua mkate akamshukuru Mungu mbele ya macho ya kila mtu. Kisha akaumega mkate akaanza kula.
36Kisha wote wakatiwa moyo na wao wakachukua chakula.
37Tulikuwa watu 276 ndani ya meli.
38Walipokwisha kula vya kutosha, waliifanya meli nyepesi kwa kutupa ngano ndani ya bahari.
39Ilipokuwa mchana, hawakuitambua nchi kavu, lakini wakaona sehemu ya nchi kavu iliyoingia majini iliyokuwa na mchanga mwingi. wakajadiliana kama wanaweza kuiendesha meli kuelekea hapo.
40Hivyo wakazilegeza nanga wakaziacha baharini. Katika muda huo huo wakazilegeza kamba za tanga na wakaiinua sehemu ya mbele kuelekea kwenye upepo, hivyo wakaelekea kwenye hiyo sehemu ya mchanga mwingi.
41Lakini wakaja mahali ambapo mikondo miwili ya maji inakutana, na meli ikaelekea mchangani. Na ile sehemu ya mbele ya meli ikakwama pale na haikuweza kutoka, lakini sehemu ya mbele ya meli ikaanza kuvunjika kwa sababu ya ukali wa mawimbi.
42Mpango wa wale askari ulikuwa ni kuwaua wafungwa, ili kwamba hakuna ambaye angeogelea na kutoroka.
43Lakini yule askari wa jeshi la Kiroma alitaka kumwokoa Paulo, hivyo akausimamisha mpango wao; na akawaamuru wale ambao wanaweza kuogelea, waruke kutoka melini kwanza na waende nchi kavu.

Read Matendo ya Mitume 27Matendo ya Mitume 27
Compare Matendo ya Mitume 27:17-43Matendo ya Mitume 27:17-43