Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Matendo ya Mitume - Matendo ya Mitume 20

Matendo ya Mitume 20:9-16

Help us?
Click on verse(s) to share them!
9Katika dirisha alikuwa amekaa kijana mmoja jina lake Utiko, ambaye alielemewa na usingizi mzito. Hata Paulo alipokuwa akihutubu kwa muda mrefu, kijana huyu, akiwa amelala, akaanguka chini kutoka ghorofa ya tatu na aliokotwa akiwa amekufa.
10Lakini Paulo alishuka chini, alijinyoosha yeye mwenyewe juu yake, akamkumbatia. Kisha akasema, “Msikate tamaa, kwa kuwa yu hai.”
11Kisha akapanda tena ghorofani na akaumega mkate, akala. Baada ya kuzungumza nao kwa muda mrefu hadi alfajiri, akaondoka.
12Wakamleta yule kijana akiwa hai wakafarijika sana.
13Sisi wenyewe tulitangulia mbele ya Paul kwa meli na tukaelekea Aso, ambapo sisi tulipanga kumchukua Paul huko. Hiki ndicho yeye mwenyewe alitaka kufanya, kwa sababu alipanga kwenda kupitia nchi kavu.
14Alipotufikia huko Aso, tukampakia kwenye Meli tukaenda Mitilene.
15Kisha sisi tukatweka kutoka huko na siku ya pili tulifika upande wa pili wa kisiwa cha Kio. Siku iliyofuata, tukawasili kisiwa cha Samo, na kesho yake tukafika mji wa Mileto.
16Kwa sababu Paulo alikuwa ameamua kusafiri kupitia Efeso, ili kwamba asitumie muda wowote katika Asia; kwa maana alikuwa na haraka ya kuwahi Yerusalemu kwa ajili ya sikukuu ya Pentekoste, kama ingeliwezekana yeye kufanya hivyo.

Read Matendo ya Mitume 20Matendo ya Mitume 20
Compare Matendo ya Mitume 20:9-16Matendo ya Mitume 20:9-16