Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Matendo ya Mitume - Matendo ya Mitume 20

Matendo ya Mitume 20:6-19

Help us?
Click on verse(s) to share them!
6kwa njia ya Bahari kutoka Filipi baada ya siku za mikate isiyotiwa chachu, na katika siku tano tukawafikia huko Troa. Tulikaa huko kwa siku saba.
7Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekusanyika pamoja ili kuumega mkate, Paulo alizungumza na Waamini. Alikuwa akipanga kuondoka kesho yake, hivyo akaendelea kuongea hadi usiku wa manane.
8Kulikuwa na taa nyingi katika chumba cha juu ambapo tulikuwa tumekusanyika pamoja.
9Katika dirisha alikuwa amekaa kijana mmoja jina lake Utiko, ambaye alielemewa na usingizi mzito. Hata Paulo alipokuwa akihutubu kwa muda mrefu, kijana huyu, akiwa amelala, akaanguka chini kutoka ghorofa ya tatu na aliokotwa akiwa amekufa.
10Lakini Paulo alishuka chini, alijinyoosha yeye mwenyewe juu yake, akamkumbatia. Kisha akasema, “Msikate tamaa, kwa kuwa yu hai.”
11Kisha akapanda tena ghorofani na akaumega mkate, akala. Baada ya kuzungumza nao kwa muda mrefu hadi alfajiri, akaondoka.
12Wakamleta yule kijana akiwa hai wakafarijika sana.
13Sisi wenyewe tulitangulia mbele ya Paul kwa meli na tukaelekea Aso, ambapo sisi tulipanga kumchukua Paul huko. Hiki ndicho yeye mwenyewe alitaka kufanya, kwa sababu alipanga kwenda kupitia nchi kavu.
14Alipotufikia huko Aso, tukampakia kwenye Meli tukaenda Mitilene.
15Kisha sisi tukatweka kutoka huko na siku ya pili tulifika upande wa pili wa kisiwa cha Kio. Siku iliyofuata, tukawasili kisiwa cha Samo, na kesho yake tukafika mji wa Mileto.
16Kwa sababu Paulo alikuwa ameamua kusafiri kupitia Efeso, ili kwamba asitumie muda wowote katika Asia; kwa maana alikuwa na haraka ya kuwahi Yerusalemu kwa ajili ya sikukuu ya Pentekoste, kama ingeliwezekana yeye kufanya hivyo.
17Kutoka Mileto akatuma watu hadi Efeso na akawaita wazee wa Kanisa.
18Walipofika kwake, akawaambia, ninyi wenyewe mwajua tangu siku ya kwanza nilipokanyaga hapa Asia, jinsi nilivyokuwa kwenu muda wote.
19Nimemtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote na kwa machozi, na mateso yaliyonipata mimi kwa hila za Wayahudi.

Read Matendo ya Mitume 20Matendo ya Mitume 20
Compare Matendo ya Mitume 20:6-19Matendo ya Mitume 20:6-19