Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Matendo ya Mitume - Matendo ya Mitume 19

Matendo ya Mitume 19:11-27

Help us?
Click on verse(s) to share them!
11Mungu alikuwa akifanya matendo makuu kwa mikono ya Paulo,
12kwamba hata wagonjwa waliponywa, na roho chafu waliwatoka, wakati walipochukua leso na nguo zilizotoka mwilini mwa Paulo.
13Lakini palikuwapo Wayahudi wapunga pepo wakisafiri kupitia eneo hilo, wakilitumia jina la Yesu kwa ajili ya matumizi yao wenyewe. Wakiwaambia wale walikuwa na pepo wachafu; Wakisema, “Ninawaamuru mtoke kwa jina la Yesu ambaye Paulo anamhubiri.”
14Waliofanya haya walikuwa wana saba wa kuhani Mkuu wa Kiyahudi, Skewa.
15Roho wachafu wakawajibu, “Yesu namjua, na Paulo namjua; lakini ninyi ni nani?
16“Yule roho mchafu ndani ya mtu akawarukia wapunga pepo na akawashinda nguvu na kuwapiga. Ndipo wakakimbia kutoka ile nyumba wakiwa uchi na kujeruhiwa.
17Jambo hili likajulikana kwa wote, Wayahudi na Wayunani, ambao waliishi huko Efeso. Wakawa na hofu sana, na jina la Bwana likazidi kuheshimiwa.
18Pia, wengi wa waumini walikuja na wakaungama na wakidhihirisha matendo mabaya waliyoyafanya.
19Wengi waliokuwa wakifanya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma mbele ya kila mtu. Wakati wao walipohesabu thamani ya vitu hivyo, ilikuwa vipande hamsini elfu vya fedha.
20Hivyo Neno la Bwana likaenea kwa upana sana katika nguvu.
21ya Paulo kukamilisha huduma yake kule Efeso, Roho akamwongoza kwenda Yerusalemu kupitia Makedonia na Akaya; Akasema, “Baada ya kuwako huko, yanipasa kuiona Rumi pia.”
22Paul akawatuma Makedonia wanafunzi wake wawili, Timotheo na Erasto, ambao walikuwa wamemsaidia. Lakini yeye mwenyewe akabaki Asia kwa muda.
23Wakati huo kulitokea ghasia kubwa huko Efeso kuhusu ile Njia.
24Sonara mmoja jina lake Demetrio, ambaye aliyetengeneza visanamu vya fedha vya mungu Diana, alileta biashara kubwa kwa mafundi.
25Hivyo akawakusanya mafundi wa kazi hiyo na kusema, “Waheshimiwa, mnajua kwamba katika biashara hii sisi tunaingiza pesa nyingi.
26Mnaona na kusikia kwamba, si tu hapa Efeso, bali karibia Asia yote, huyu Paulo amewashawishi na kuwageuza watu wengi. Anasema kwamba hakuna miungu ambayo imefanywa kwa mikono.
27Na si tu iko hatari kwamba biashara yetu itakuwa haihitajiki tena, lakini pia na hekalu la mungu mke aliye mkuu Diana anaweza kuchukuliwa kuwa hana maana. Tena angeweza hata kupoteza ukuu wake, yeye ambaye Asia na dunia humwabudu.”

Read Matendo ya Mitume 19Matendo ya Mitume 19
Compare Matendo ya Mitume 19:11-27Matendo ya Mitume 19:11-27