Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Matendo ya Mitume - Matendo ya Mitume 15

Matendo ya Mitume 15:27-40

Help us?
Click on verse(s) to share them!
27Kwa hiyo tumemtuma Yuda na Sila, watawaambia mambo yayo hayo.
28Kwa kuwa ilionekana vyema kwa Roho Mtakatifu na kwetu, kutoweka juu yenu mzigo mkubwa kuliko mambo haya yaliyo ya lazima:
29kwamba mgeuke kutoka kwenye vitu vitolewavyo kwa sanamu, damu, vitu vya kunyongwa, na uasherati. Kama mtajiweka mbali na hivi, itakuwa vyema kwenu. Kwa herini.”
30Hivyo basi, walivyotawanyishwa, waliteremkia Antiokia; baada ya kukusanya kusanyiko pamoja, waliwasilisha barua.
31Walipokua wameisoma, walifurahi kwa sababu ya kutiwa moyo.
32Yuda na Sila, na manabii, waliwatia moyo ndugu kwa maneno mengi na kuwatia nguvu.
33Baada ya kukaa muda fulani huko, walitawanyishwa kwa amani kutoka kwa ndugu kwa wale waliowatuma.
34Lakini ilionekana vyema Sila kubaki huko
35Lakini Paulo na wengine walikaa Antiokia pamoja na wengine wengi, ambapo walifundisha na kuhubiri neno la Bwana.
36Baada ya siku kadhaa Paulo alisema kwa Barnaba, “Na turudi sasa na kuwatembelea ndugu katika kila mji tulipohubiri neno la Bwana, na kuwaona walivyo.
37Barnaba alihitaji pia kumchukua pamoja nao Yohana aliyeitwa Marko.
38Lakini Paulo alifikiria haikuwa vizuri kumchukua Marko, aliyewaacha huko Pamfilia na hakuendelea nao katika kazi.
39Kisha hapo kukatokea mabishano makubwa kwa hiyo walitengana, na Barnaba alimchukua Marko na kusafiri kwa meli mpaka Kipro,
40Lakini Paulo alimchagua Sila na kuondoka, baada ya kukabidhiwa na ndugu katika neema ya Bwana.

Read Matendo ya Mitume 15Matendo ya Mitume 15
Compare Matendo ya Mitume 15:27-40Matendo ya Mitume 15:27-40