Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Matendo ya Mitume - Matendo ya Mitume 13

Matendo ya Mitume 13:40-52

Help us?
Click on verse(s) to share them!
40Hivyo basi kuweni waangalifu kwamba kitu walichokiongelea manabii kisitokee kwenu:
41'Tazama, enyi mnaodharau, na mkashangae na mkaangamie; kwa vile nafanya kazi katika siku zenu, Kazi ambayo hamwezi kuiamini, hata kama mtu atawaeleza.”
42Wakati Paulo na Barnaba walipoondoka, watu wakawaomba waongee maneno haya siku ya Sabato ijayo.
43Wakati mkutano wa sinagogi ulipokwisha, Wayahudi wengi na waongofu thabiti waliwafuata Paulo na Barnaba, ambao waliongea nao na waliwahimiza waendelee katika neema ya Mungu.
44Sabato iliyofuata, karibu mji mzima ulikusanyika kusikia neno la Mungu.
45Wayahudi walipoona makutano, walijawa na wivu na kuongea maneno yaliyopinga vitu vilivyosemwa na Paulo na walimtukana.
46Lakini Paulo na Barnaba waliongea kwa ujasiri na kusema, “Ilikuwa ni muhimu kwamba neno la Mungu liongelewe kwanza kwenu. Kwa kuwa mnalisukumia mbali kutoka kwenu nakujiona kuwa hamkusitahili uzima wa milele, angalieni tutawageukia Mataifa.
47Kama ambavyo Bwana ametuamuru, akisema, 'Nimewaweka ninyi kama nuru kwa watu wa mataifa, kwamba mlete wokovu kwa pande zote za dunia.”
48Mataifa waliposikia hili, walifurahi na kulisifu neno la Bwana. Wengi waliochaguliwa kwa uzima wa milele waliamini.
49Neno la Bwana lilienea nchi yote.
50Lakini wayahudi waliwasihi waliojitoa na wanawake muhimu, pia na viongozi wa mji. Haya yalichochea mateso dhidi ya Paulo na Barnaba na waliwatupa nje ya mipaka ya mji.
51Lakini Paulo na Barnaba walikung'uta vumbi ya miguu yao. Kisha walienda kwenye mji wa Ikonia.
52Na wanafunzi walijawa na furaha pamoja na Roho mtakatifu.

Read Matendo ya Mitume 13Matendo ya Mitume 13
Compare Matendo ya Mitume 13:40-52Matendo ya Mitume 13:40-52