Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Matendo ya Mitume - Matendo ya Mitume 12

Matendo ya Mitume 12:5-23

Help us?
Click on verse(s) to share them!
5Petro akawekwa gerezani, lakini maombi yakafanywa kwa bidii na kusanyiko kwa ajili yake kwa Mungu.
6Siku kabla Herode hajaenda kumtoa, Usiku huo Petro alikuwa amelala katikati ya maaskari wawili, akiwa amefungwa na minyororo miwili, na walinzi mbele ya mlango walikuwa wakilinda gereza.
7Tazama, malaika wa Bwana ghafla akamtokea na nuru ikang'aa ndani. Akampiga Petro ubavuni na kumwamsha akisema, “Amka haraka.” ndipo minyororo aliyokuwa amefungwa ikafunguka kutoka mikononi mwake.
8Malaika akamwambia, “Vaa nguo zako na vaa viatu vyako.” Petro akafanya hivyo. Malaika akamwambia, “Vaa vazi lako na unifuate.”
9Hivyo Petro akamfuata Malaika na akatoka nje. Hakuamini kilichofanywa na malaika kama ni cha kweli. Alidhani anaona maono.
10Baada ya kupita lindo la kwanza na la pili, wakafika kwenye geti la chuma la kuingilia kwenda mjini, likafunguka lenyewe kwa ajili yao. Wakatoka nje wakashuka kwenye mtaa, mara Malaika akamwacha.
11Petro alipojitambua, akasema, “Sasa nimeamini kuwa Bwana alimtuma Malaika wake ili kunitoa katika mikono ya Herode, na kwa matarajio ya watu wote wa uyahudi.”
12Baada ya kujua haya, akaja kwenye nyumba ya Mariamu mama yake Yohana ambaye ni Marko; Wakristo wengi walikusanyika wakiomba.
13Alipobisha kwenye mlango wa kizuizi, mtumishi mmoja msichana anayeitwa Roda akaja kufungua.
14Alipotambua ni sauti ya Petro, kwa furaha akashindwa kuufungua mlango; badala yake, akakimbia ndani ya chumba; na kuwajulisha kuwa Petro amesimama mbele ya Mlango.
15Hivyo, Wakasema kwake, “Wewe ni mwendawazimu” lakini alikazia kuwa ni kweli ni yeye. Wakasema “Huyo ni malaika wake.”
16Lakini Petro aliendelea kubisha, na walipofungua mlango, wakamwona na wakashangaa sana. Petro akawanyamazisha kwa mkono kimya kimya na akawaambia jinsi Bwana alivyomtoa kutoka Gerezani. akasema,
17“Wajulishe haya mambo Yakobo na ndugu zake.” Kisha akaondoka akaenda sehemu nyingine.
18Kulipokuwa mchana, kukawa na huzuni kubwa kati ya askari, kuhusiana na kilichotokea kwa Petro.
19Baada ya Herode kumtafuta na hakumwona akawauliza walinzi na akaamuru wauawe. Akaenda kutoka uyahudi mpaka Kaisaria na kukaa huko.
20Herode alikuwa na hasira juu ya watu wa Tiro na Sidoni. Wakaenda kwa pamoja kwake. Wakawa na urafiki na Blasto msaidizi wa mfalme, ili awasaidie. Kisha wakaomba amani, kwa sababu nchi yao ilipokea chakula kutoka katika nchi ya mfalme.
21Siku iliyokusudiwa Herode alivaa mavazi ya kifalme na kukaa kwenye kiti chake cha kifalme, na akawahutubia.
22Watu wakapiga kelele, “Hii ni sauti ya mungu wala si sauti ya mwanadamu!”
23Mara ghafla malaika akampiga, kwa sababu alikuwa hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na chango na akafa

Read Matendo ya Mitume 12Matendo ya Mitume 12
Compare Matendo ya Mitume 12:5-23Matendo ya Mitume 12:5-23