Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Matendo ya Mitume - Matendo ya Mitume 12

Matendo ya Mitume 12:17-25

Help us?
Click on verse(s) to share them!
17“Wajulishe haya mambo Yakobo na ndugu zake.” Kisha akaondoka akaenda sehemu nyingine.
18Kulipokuwa mchana, kukawa na huzuni kubwa kati ya askari, kuhusiana na kilichotokea kwa Petro.
19Baada ya Herode kumtafuta na hakumwona akawauliza walinzi na akaamuru wauawe. Akaenda kutoka uyahudi mpaka Kaisaria na kukaa huko.
20Herode alikuwa na hasira juu ya watu wa Tiro na Sidoni. Wakaenda kwa pamoja kwake. Wakawa na urafiki na Blasto msaidizi wa mfalme, ili awasaidie. Kisha wakaomba amani, kwa sababu nchi yao ilipokea chakula kutoka katika nchi ya mfalme.
21Siku iliyokusudiwa Herode alivaa mavazi ya kifalme na kukaa kwenye kiti chake cha kifalme, na akawahutubia.
22Watu wakapiga kelele, “Hii ni sauti ya mungu wala si sauti ya mwanadamu!”
23Mara ghafla malaika akampiga, kwa sababu alikuwa hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na chango na akafa
24Lakini neno la Mungu likakua na kusambaa.
25Baada ya Barnaba na Sauli kukamilisha huduma yao wakatoka pale wakarejea Yerusalemu, wakamchukua na Yohana ambaye jina la kuzaliwa ni Marko.

Read Matendo ya Mitume 12Matendo ya Mitume 12
Compare Matendo ya Mitume 12:17-25Matendo ya Mitume 12:17-25