Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Matendo ya Mitume - Matendo ya Mitume 10

Matendo ya Mitume 10:8-24

Help us?
Click on verse(s) to share them!
8Kornelio aliwaambia yote yaliyotokea na akawatuma Yafa.
9Siku iliyofuata muda wa saa sita wakiwa njiani na wamekaribia mjini, Petro akapanda juu darini kuomba.
10Na pia akawa na njaa na alihitaji kitu cha kula, lakini wakati watu wanapika chakula, akaonyeshwa maono,
11akaona anga limefuguka na chombo kinashuka na kitu fulani kama nguo kubwa ikishuka chini kwenye ardhi katika kona zake zote nne.
12Ndani yake kulikuwa na aina zote za wanyama wenye miguu minne na watambaao juu ya ardhi, na ndege wa angani.
13Tena sauti ikasema kwake “Amka, Petro chinja na ule”.
14Lakini Petro akasema “Siyo hivyo, Bwana kwa sababu sijawahi kula kitu chochote najisi na kichafu.
15Lakini sauti ikaja kwake tena kwa mara ya pili “Alichokitakasa Mungu usikiite najisi wala kichafu”.
16Hii ilitokea mara tatu, na kile chombo kikawa kimechukuliwa tena angani.
17Na wakati Petro akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa juu ya hayo maono yanamaanisha nini, Tazama, watu waliokuwa wametumwa na Kornelio wakasimama mbele ya lango, wakiuliza njia ya kwenda kwenye nyumba.
18Na wakaita na kuuliza kama Simoni ambaye pia aliitwa Petro kama alikuwa anakaa pale.
19Wakati huo Petro alipokuwa akiwaza juu ya hayo maono, Roho akasema naye, “Tazama watu watatu wanakutafuta.
20Amka na ushuke chini na uende nao. Usiogope kwenda nao, kwa sababu nimewatuma.”
21Petro akashuka chini kwao na kusema “Mimi ni yule mnayemtafuta. Kwa nini mmekuja?”
22Wakasema, “Akida mmoja jina lake Kornelio, mtu wa haki na hupenda kumwabudu Mungu, na watu humsema vyema katika taifa lote la kiyahudi, ameambiwa na malaika wa Mungu kukutuma ili kwenda kwenye nyumba yake, ili asikie ujumbe kutoka kwako.”
23Petro akawakaribisha kuingia ndani na kukaa pamoja naye. Asubuhi iliyofuata akaamka akaenda pamoja naye, na ndugu wachache kutoka Yafa wakaambatana naye.
24Siku iliyofuata walikuja Kaisaria. Na Kornelio alikuwa akiwasubiri; na alikuwa amewaita pamoja ndugu zake na marafiki zake wa karibu.

Read Matendo ya Mitume 10Matendo ya Mitume 10
Compare Matendo ya Mitume 10:8-24Matendo ya Mitume 10:8-24