Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Matendo - Matendo 1

Matendo 1:3-6

Help us?
Click on verse(s) to share them!
3Kwa muda wa siku arobaini baada ya kifo chake aliwatokea mara nyingi kwa namna ambazo zilithibitisha kabisa kwamba alikuwa hai. Walimwona, naye aliongea nao juu ya ufalme wa Mungu.
4Wakati walipokutana pamoja aliwaamuru hivi: “Msiondoke Yerusalemu, bali ngojeeni ile zawadi aliyoahidi Baba, zawadi ambayo mlikwisha nisikia nikiongea juu yake.
5Kwani Yohane alibatiza kwa maji, lakini baada ya siku chache, ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.”
6Basi, mitume walipokutana pamoja na Yesu, walimwuliza, “Je Bwana, wakati huu ndipo utakaporudisha ule ufalme kwa Israeli?”

Read Matendo 1Matendo 1
Compare Matendo 1:3-6Matendo 1:3-6