Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Matendo - Matendo 14

Matendo 14:16-26

Help us?
Click on verse(s) to share them!
16Zamani Mungu aliruhusu kila taifa lifanye lilivyopenda.
17Hata hivyo, Mungu hakuacha kujidhihirisha kwa mambo mema anayowatendea: huwanyeshea mvua toka angani, huwapa mavuno kwa wakati wake, huwapa chakula na kuijaza mioyo yenu furaha.”
18Ingawa walisema hivyo haikuwa rahisi kuwazuia wale watu wasiwatambikie.
19Lakini Wayahudi kadhaa walikuja kutoka Antiokia na Ikonio, wakawafanya watu wajiunge nao, wakampiga mawe Paulo na kumburuta hadi nje ya mji wakidhani amekwisha kufa.
20Lakini waumini walipokusanyika na kumzunguka, aliamka akarudi mjini. Kesho yake, yeye pamoja na Barnaba walikwenda Derbe.
21Baada ya Paulo na Barnabas kuhubiri Habari Njema huko Derbe na kupata wafuasi wengi, walifunga safari kwenda Antiokia kwa kupitia Lustra na Ikonio.
22Waliwaimarisha waumini wa miji hiyo na kuwatia moyo wabaki imara katika imani. Wakawaambia, “Ni lazima sisi sote tupitie katika taabu nyingi ili tuingie katika ufalme wa Mungu.”
23Waliteua wazee katika kila kanisa kwa ajili ya waumini, na baada ya kusali na kufunga, wakawaweka chini ya ulinzi wa Bwana ambaye walikuwa wanamwamini.
24Baada ya kupitia katika nchi ya Pisidia, walifika Pamfulia.
25Baada ya kuhubiri ule ujumbe huko Perga, walikwenda Atalia.
26Kutoka huko walisafiri kwa meli wakarudi Antiokia ambako hapo awali walikuwa wamewekwa chini ya ulinzi wa neema ya Mungu kwa ajili ya kazi ambayo sasa walikuwa wameitimiza.

Read Matendo 14Matendo 14
Compare Matendo 14:16-26Matendo 14:16-26