Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Marko - Marko 8

Marko 8:5-17

Help us?
Click on verse(s) to share them!
5Yesu akawauliza, “Mnayo mikate mingapi?” Nao wakamjibu, “Saba.”
6Basi, akawaamuru watu wakae chini. Akaitwaa ile mikate saba, akamshukuru Mungu, akaimega, akawapa wanafunzi wake wawagawie watu, nao wakawagawia.
7Walikuwa pia na visamaki vichache. Yesu akavibariki, akaamuru vigawiwe watu vilevile.
8Watu wakala, wakashiba. Wakaokota mabaki yaliyosalia wakajaza makapu saba.
9Nao waliokula walikuwa watu wapatao elfu nne. Yesu akawaaga,
10na mara akapanda mashua pamoja na wanafunzi wake, akaenda wilaya ya Dalmanutha.
11Mafarisayo walikuja, wakaanza kujadiliana na Yesu. Kwa kumjaribu, wakamtaka awafanyie ishara kuonyesha anayo idhini kutoka mbinguni.
12Yesu akahuzunika rohoni, akasema, “Mbona kizazi hiki kinataka ishara? Kweli nawaambieni, kizazi hiki hakitapewa ishara yoyote!”
13Basi, akawaacha, akapanda tena mashua, akaanza safari kwenda ng'ambo ya pili ya ziwa.
14Wanafunzi walikuwa wamesahau kuchukua mikate; walikuwa na mkate mmoja tu katika mashua.
15Yesu akawaonya, “Angalieni sana! Jihadharini na chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode.”
16Wanafunzi wakaanza kujadiliana wao kwa wao, “Anasema hivyo kwa kuwa hatuna mikate.”
17Yesu alitambua hayo, akawaambia, “Mbona mnajadiliana juu ya kutokuwa na mikate? Je, bado hamjafahamu, wala hamjaelewa? Je, mioyo yenu imeshupaa?

Read Marko 8Marko 8
Compare Marko 8:5-17Marko 8:5-17