Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 8

Mambo ya Walawi 8:1-22

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Yahweh akazungumza na Musa, akisema,
2“Walete Aroni na wanawe pamoja naye, mavazi na mafuta ya upako, fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi, kondoo dume wawili, na kikapu cha mkate usio na hamira.
3Ita kusanyiko lote kwenye ingilio la hema la kukutania.”
4Kwa hiyo Musa akafanya kama Yahweh alivyomwamru, nalo kusanyiko lilikuja pamoja mbele ya ingilio la hema la kukutania. Kisha Musa akaliambia kusanyiko,
5“Hivi ndivyo alivyotuamru Yahweh tutende.”
6Musa akamleta Aroni na wanawe na kuwaosha kwa maji.
7Akamvika Aroni kanzu ya ndani yenye urefu wa kufika magotini na kumfunga ukumbuu kiunoni mwake, akamvika joho la nje lenye mikono mirefu na kumvika kile kizibao chenye vipande viwili tumboni na mgongoni na kukifunga kuzunguka kiunoni mwake kwa mshipi uliosokotwa kwa ustadi na kukikaza mwilini mwake.
8Kisha Musa akaweka kifuko kifuani mwa Aroni, na ndani ya kifuko hicho akaweka Urimu na Thumimu.
9Na kisha akamfunga kiremba kichwani, na juu ya kiremba kwa mbele, akaweka bamba la dhahabu; liwe taji takatifu, kama Yahweh alivyomwamru yeye.
10Musa akayatwaa hayo mafuta ya upako, akalipaka lile hema la kukutania na kila kitu kilichokuwamo ndani yake na kuvitenga kwa ajili ya Yahweh.
11Akayanyunyiza hayo mafuta juu ya madhabahu mara saba, na kisha akaipaka mafuta hiyo madhabahu na vyombo vyake vyote, na sinia la kunawia na kitako chake ili kuvitenga wa ajili ya Yahweh.
12Akamimina sehemu ya mafuta ya upako juu ya kichwa cha Aroni na kisha akampaka mafuta ili kumtenga.
13Musa akawaleta wana wa Aroni na kuwavika kila mmoja kanzu ya ndani yenye urefu wa kufika magotini. Kila mmoja wao akamfunga kwa ukumbuu kiunoni mwake na kuwafunga vitambaa vya kitani kichwani pao, kama vile Yahweh alivyokuwa amemru Musa.
14Musa akamleta huyo fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi, naye Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa cha fahali ambaye wamemelete kwa ajili ya sadaka ya dhambi.
15Musa akamchinja, na kisha akachukua sehemu ya damu yake kwa kidole chake na kuiweka juu ya mpembe za madhabahu, akaitakasa hiyo madhabahu, na kuitenga kwa Mungu, ambapo kwa kufanya hivyo, aliisababisha madhabahu kuwa sehemu ya kufaa kwa kufanyia upatanisho.
16Akachukua mafuta yote yaliyokuwa sehemu za ndani, kile kiwambo cha ini, zile figo mbili pamoja na mafuta yake, Musa akaichoma hiyo nyama yote juu ya madhabahu.
17Lakini yule fahali, ngozi yake, nyama yake na kinyesi chake, akavichoma nje ya kambi, kama vile Yehweh alivyokuwa amemwamru yeye.
18Musa akamleta yule konndoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, naye Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa cha huyo kondoo.
19Musa akamchinja kondoo na kuinyunyizia damu yake kila upande wa madhabahu.
20Naye akamkatakata kondoo vipande vipande na akakiteketeza kichwa chake pamoja na vile vipande na mafuta.
21Akaziosha kwa maji zile sehemu za ndani pamoja na miguu na akamteketeza kandoo mzima juu ya madhabahu. Ilikuwa ni dhabihu ya kuteketezwa na ilitoa harufu ya kupendeza, sadaka iliyofanywa kwa Yahweh kwa moto kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamru Musa.
22Kisha Musa akamleta yule kondoo dume mwingine, kondoo wa kuwekwa wakfu, naye Aroni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa cha kondoo.

Read Mambo ya Walawi 8Mambo ya Walawi 8
Compare Mambo ya Walawi 8:1-22Mambo ya Walawi 8:1-22