Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 7

Mambo ya Walawi 7:24-37

Help us?
Click on verse(s) to share them!
24Mafuta ya mnyama yoyote afaye peke yake bila ya kuwa dhabihu, au mafuta ya mnyama yeyote aliyeraruliwa na wanyama pori, yanaweza kutumika kwa makusudi mengine, lakini hakika hamtayala.
25Yeyote atakayekula mafuta ya mnyama ambayo watu wanaweza kuyatoa kuwa dhabihu ya iliyofanywa kwa Yahweh kwa moto, mtu huyo lazima atakatiliwa mbali kutoka kwa watu wake.
26Hamtakula damu yoyote katika mojawapo ya nyumba zenu, ama iwe kutoka kwa ndege au mnyama.
27Yeyote alaye damu yoyote, mtu huyo lazima akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.'”
28Kwa hiyo Yahweh akazungumza na Musa na akasema,
29“Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, 'Yeye atoaye dhabidhu ya sadaka ya amani kwa Yahweh lazima alete sehemu ya dhabihu yake kwa Yahweh.
30Mikono yake mwenyewe lazima iilete hiyo sadaka ifanywayo kwa Yahweh kwa moto. Naye atayaleta hayo mafuta pamoja na kidari, ili kwamba kidari kiweze kutikiswa kuwa sadaka ya kutikiswa mbele za Yahweh.
31Kuhani atayachoma mafuta hayo juu ya madhabahu, lakini kile kidari kitakuwa mali ya Aroni na uzao wake.
32Ni lazima utatoa paja la kulia kwa kuhani kama sadaka iliyotokana na dhabihu ya sadaka yako ya amani.
33Yule kuhani, mmoja wa wazao wa Aroni, atoaye damu na mafuta ya sadaka ya amani—ni lazima atapata paja la kulia kama mgao wake wa sadaka.
34Kwa kuwa nimetwaa kidari, na paja la sadaka ya kutikiswa kutoka kwa watu wa Israeli uwe mchango wao, na amepewa Aroni kuhani na wanawe kuwa mgao wao wa kawaida.
35Huu ndiyo mgao wa Aroni na uzao wake utokanao na matoleo yaliyofanywa kwa Yahweh kwa moto, siku ile Musa alipowaweka wakfu ili kumtumikia Yahweh katika kazi ya kuhani.
36Huu ndio mgao ambao Yahweh aliamru waweze kupewa kutoka kwa watu wa Israeli, katika siku hiyo aliyowatia mafuta ya upako wawe makuhani. Nao utakuwa mgao wao wa kila siku katika vizazi vyote.
37Hii ndiyo sheria ya sadaka ya kuteketezwa, ya sadaka ya nafaka, ya sadaka ya dhambi, ya sadaka ya hatia, ya sadaka ya kuweka wakfu, na ya dhabihu, ya sadaka za amani,

Read Mambo ya Walawi 7Mambo ya Walawi 7
Compare Mambo ya Walawi 7:24-37Mambo ya Walawi 7:24-37