Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 5

Mambo ya Walawi 5:8-13

Help us?
Click on verse(s) to share them!
8Atawaleta kwa kuhani, wa kwanza atatoa kwa ajili ya sadaka ya dhambi. Atamvunja shingo yake lakini ataacha kichwa chake kinaning'inia wala hataiondoa kabisa shingo yake katika mwili.
9Ndipo atanyunyizia damu yake katika sehemu za madhabahu, na damu inayobaki ataimwaga chini ya madhabahu. Hii ni dhabihu ya dhambi.
10Ndipo ataoa ndege wa pili kama sadaka ya kuteketezwa kama ilivyoelekezwa, na kuhani atafanya upatanisho kwa ajili ya dhambi alizokwisha kufanya, na huyo mtu atakuwa amesamehewa.
11Lakini kama hataweza kununua hua wawili au makinda ya njiwa mawili, ndipo ataleta kama dhabihu ya dhambi zake sehemu ya kumi ya unga laini kama sadaka ya dhambi. Asiweke mafuta wala ubani juu yake, kwa kuwa ni sadaka ya dhambi.
12Atauleta kwa kuhani, na kuhani atachukua konzi moja ya unga kama ukumbusho wa wema wa Bwana na atauweka juu ya madhabahu na kuteketeza juu ya sadaka za kuteketezwa kwa moto kwa ajili ya Bwana. Hii ni sadaka ya dhambi.
13Kuhani atafanya upatanisho kwa dhambi yoyote aliyofanya mtu yeyote, mtu huyo atasamehewa. Na sadaka inayobaki itakuwa ya kuhani, kama ilivyo sadaka ya nafaka.'”

Read Mambo ya Walawi 5Mambo ya Walawi 5
Compare Mambo ya Walawi 5:8-13Mambo ya Walawi 5:8-13