Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 4

Mambo ya Walawi 4:8-26

Help us?
Click on verse(s) to share them!
8Atakata mafuta yote ya dume wa sadaka ya dhambi, mafuta yanayofunika matumbo na mafuta yote yaliyo katika matumbo,
9figo mbili na mafuta yaliyopo pamoja nazo, yaliyo karibu na kiuno na kitambi cha maini pamoja na hizo figo.
10Ataondoa zote vile vile kama yanavyoondolewa katika dume wa sadaka ya dhabihu ya amani. Kuhani atatekeza sehemu hizo katika madhabahu ya sadaka za kuteketezwa.
11Ngozi ya dume na mabaki yoyote ya nyama, pamoja na kichwa chake, miguu yake, matumbo yake na mavi yake,
12mabaki yote ya dume atayachukua nje ya mji mahali palipo safi, mahali wanapomwaga majivu; watateketeza sehemu zote juu ya kuni. Watateketeza sehemu zote mahali wanapomwaga majivu.
13Kama mkutano wote wa wana wa Israeli wakitenda dhambi bila kukusudia, na mkutano hawatakumbuka kwamba wametenda dhambi, na kufanya vile Bwana aliagiza wasifanye na wakajisikia hatia.
14Na dhambi waliyofanya ikajulikana, mkutano watatoa ng'ombe dume mchanga kuwa sadaka ya dhambi watamleta mbele ya hema ya kukutania.
15Wazee wa mkutano wataweka mikono yao juu ya kichwa cha ng'ombe mbele za Bwana, na ng'ombe atachinjwa mbele za Bwana.
16Kuhani aliyetiwa mafuta ataleta damu ya ng'ombe katika hema ya kukutania,
17kuhani atachovya kidole chake katika damu na kuinyunyizia mara saba mbele za Bwana mbele ya pazia.
18Ataweka kiasi cha damu katika pembe za madhabahu mbele za Bwana iliyo katika hema ya kukutania na ataimwaga damu yote chini ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo katika mlango wa kuingilia katika hema ya kukutania.
19Atakata mafuta yote na kuyatekeza katika madhabahu.
20Hivyo ndivyo atakavyomfanya huyo ng'ombe, kama alivyomfanya ng'ombe wa sadaka ya dhambi, atamfanyia vivyo hivyo huyu ng'ombe, kuhani atawafanyia upatanisho watu nao watasamehewa.
21Atamchukua huyo ng'ombe nje ya mji na kumteketeza kama alivyomteketeza ng, ombe wa kwanza. Hii ni sadaka ya dhambi kwa ajili ya mkutano.
22Mtawala akitenda dhambi bila kukusudia kufanya moja ya yale Bwana Mungu wake ameagiza kutotenda, na anajisikia hatia
23na kama dhambi yake aliyotenda anaifahamu, ataleta dhabihu yake mbuzi mme asiye na kasoro.
24Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha mbuzi na kumchinja mahali ambapo huchinja sadaka ya kuteketezwa mbele za Bwana. Hii ni sadaka ya dhambi.
25Kuhani atachukua damu ya sadaka ya dhambi kwa kidole chake na kuiweka juu ya pembe za madhabahu kwa dhabihu ya kuteketezwa, na atamwaga damu chini ya madhabahu ya dhabihu ya kuteketezwa.
26Atateketeza mafuta yote katika madhabahu, kama vile mafuta ya dhabihu ya sadaka ya amani, Kuhani atafanya upatanisho kwa ajili ya mtawala kulingana na dhambi yake, na mtawala atakuwa amesamehewa.

Read Mambo ya Walawi 4Mambo ya Walawi 4
Compare Mambo ya Walawi 4:8-26Mambo ya Walawi 4:8-26