Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 27

Mambo ya Walawi 27:18-28

Help us?
Click on verse(s) to share them!
18Lakini endapo atalitenga shamba hilo baada ya mwaka wa Yubile, kisha kuhani atalazimika kukokotoa thamani yake kwa idadi ya miaka inayobaki mpaka mwaka wa Yubile, na thamani yake lazima ishushwe.
19Iwapo mtu anayelitenga shamba lake anapenda kuliko, mboa, naye atalazimika kuongeza sehemu ya tano kwenye thamani, nalo shamba litakuwa lake tena.
20Iwapo halikomboi shamba, au iwapo amishaliuza shamba kwa mtu mwingine, haliwezi kukombolewa tena.
21Badala yake, shamba hilo litakapoachwa huru katika mwaka wa Yubile, litakuwa zawadi takatifu kwa Yahweh, kama lilivyo shamba lililotolewa kabisa kwa Yahweh. Nalo litakuwa mali ya kuhani.
22Iwapo mtu anatenga shamba alilolinunua, lakini hilo shamba siyo sehemu ya ardhi ya familia yake,
23kuhani atafanya tathmini yake mpaka mwaka wa Yubile, na mtu huyo lazima atalipa thamani yake katika siku hiyo hiyo kuwa zawadi takatifu kwa Yahweh.
24Katika mwaka wa Yubile, shamba litarejeshwa kwa mtu yule ambaye lilikuwa limenunuliwa, kwa mmiliki wa ardhi.
25Tathmani yote lazima ifanywe kwa uzani wa shekeli ya mahali pa patakatifu. Gera ishirini kwa shekeli moja.
26Asiwepo mtu atakayetenga mzaliwa wa kwanza miongoni mwa wanyama, kwa kuwa wazaliwa wote wa kwanza wa wanyama tayari ni mali ya Yahweh; iwe ni maksai au kondoo, ni wa Yahweh.
27Na kama ni mnyama aliye najisi, kisha mmiliki wake anaweza kumnunua tena sawasawa na thamani yake, na sehemu ya tano lazima itaongezwa kwenye thamani hiyo. Na kama mnyama hakombolewi, naye atauzwa kwa thamani iliyowekwa.
28Hakutakuwa na kitu amabacho mtu anakitoa kwa Yahweh, kutoka katika vyote alivyonavyo, iwe ni mwanadamu au mnyama, au ardhi ya familia yake, ambacho chaweza kuuzwa au kukombolewa. Kila kitu kitolewacho ni kitakatifu sana kwa Yahweh.

Read Mambo ya Walawi 27Mambo ya Walawi 27
Compare Mambo ya Walawi 27:18-28Mambo ya Walawi 27:18-28