Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 27

Mambo ya Walawi 27:1-30

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Yahweh akazungumza na Musa na akasema,
2“Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, 'Iwapo mtu yeyote anatoa kiapo maalum cha kuwa mnathiri kwa Yahweh, tumieni tathmini zifuatazo:
3Viwango vyenu vya thamani kwa mwanaume aliye na umri kati ya miaka ishirini na miaka sitini yaweza kuwa shekeli hamsini za fedha, kulingana na vipimo vya shekeli ya mahali pa patakatifu.
4Kwa mwanamke wa umri uleule viwango vyenu vya thamani yapasa viwe shekeli thelathini vya fedha.
5Tangu wenye umri wa miaka mitano mpaka wa miaka ishirini viwango vyenu vya thamani kwa mwananume vitakuwa shekeli ishirini za fedha, na kwa mwanamke ni shekeli kumi za fedha,
6Kwa wenye umri wa tangu mwezi mmoja mpaka miaka mitano viwango vyenu vya thamani kwa mawanaume vitakuwa shekeli tano za fedha na kwa mwanamke shekeli tatu za fedha.
7Tangu wenye umri wa miaka sitini na zaidi kwa mwanaume viwango vyenu vya thamani vitakuwa shekeli kumi na tano, na kwa mwanamke ni shekeli kumi.
8Lakini kama mtu atoaye kiapo cha mnadhiri hawezi kulipa kiwango hicho cha thamani, kisha huyo mtu anayetolewa lazima atapelekwa kwa kuhani, naye kuhani atamthamanisha huyo atolewaye kwa kiasi anachoweza kutoa yule anayetoa kiapo cha mnadhiri.
9Iwapo mtu anataka kutoa sadaka ya mnyama kwa Yahweh, na iwapo Yahweh ataikubali, kisha huyo mnyama atatengwa kwake.
10Mtu huyo hataruhusiwa kumtoa madhabahuni au kumbadilisha huyo mnyama, mzuri kwa mbaya au mbaya kwa mzuri. endapo atatoa mnyama badala ya mwingine, kisha wanyama hao wawili; yule anayetolewa na yule anayebadilishwa wanakuwa watakatifu.
11Hata hivyo, iwapo kile mtu amishaapa kumtolea Yahweh kwa uhalisia siyo kisafi, kwa hiyo, Yahweh hatakikubali, naye huyo mtu atalazimika kumleta huyo mnyama kwa kuhani.
12Kuhani atamthamanisha, kwa thamani ya soko la mnyama. Thamani yoyote kuhani atakayoiweka juu ya mnyama, hiyo ndiyo itakuwa thamani yake.
13Na kama mmiliki anapenda kumkomboa, kisha tano ya thamani yake itaongezwa kwenye gharama yake ya ukombozi.
14Mtu aitengapo nyumba yake iwe zawadi takatifu kwa Yahweh, kisha kuhani ataweka thamani yake ama iwe ni nzuri au mbaya. Thamani yoyote itakayowekwa na kuhani juu yake, ndiyo itakuwa thamani yake.
15Lakini kama mmiliki wake anayeitenga nyumba yake anapenda kuikomboa, atalazimika kuongeza sehemu ya tano ya thamani yake kwenye gharama ya ukombozi wake, nayo nyumba itakuwa yake.
16Iwapo mtu anatenga sehemu ya ardhi yake mwenye, kisha tathmini yake itakuwa katika uwiano kwa kiwango cha kiasi cha mbegu inayotakiwa kuipanda katika ardhi hiyo—homeri moja ya mbegu za shairi ambayo itathamanishwa kwa shekeli hamsini za fedha.
17Na kama analitenga shamba lake katika mwaka wa Yubile, tathmini yake ya awali itabaki kuwa ileile.
18Lakini endapo atalitenga shamba hilo baada ya mwaka wa Yubile, kisha kuhani atalazimika kukokotoa thamani yake kwa idadi ya miaka inayobaki mpaka mwaka wa Yubile, na thamani yake lazima ishushwe.
19Iwapo mtu anayelitenga shamba lake anapenda kuliko, mboa, naye atalazimika kuongeza sehemu ya tano kwenye thamani, nalo shamba litakuwa lake tena.
20Iwapo halikomboi shamba, au iwapo amishaliuza shamba kwa mtu mwingine, haliwezi kukombolewa tena.
21Badala yake, shamba hilo litakapoachwa huru katika mwaka wa Yubile, litakuwa zawadi takatifu kwa Yahweh, kama lilivyo shamba lililotolewa kabisa kwa Yahweh. Nalo litakuwa mali ya kuhani.
22Iwapo mtu anatenga shamba alilolinunua, lakini hilo shamba siyo sehemu ya ardhi ya familia yake,
23kuhani atafanya tathmini yake mpaka mwaka wa Yubile, na mtu huyo lazima atalipa thamani yake katika siku hiyo hiyo kuwa zawadi takatifu kwa Yahweh.
24Katika mwaka wa Yubile, shamba litarejeshwa kwa mtu yule ambaye lilikuwa limenunuliwa, kwa mmiliki wa ardhi.
25Tathmani yote lazima ifanywe kwa uzani wa shekeli ya mahali pa patakatifu. Gera ishirini kwa shekeli moja.
26Asiwepo mtu atakayetenga mzaliwa wa kwanza miongoni mwa wanyama, kwa kuwa wazaliwa wote wa kwanza wa wanyama tayari ni mali ya Yahweh; iwe ni maksai au kondoo, ni wa Yahweh.
27Na kama ni mnyama aliye najisi, kisha mmiliki wake anaweza kumnunua tena sawasawa na thamani yake, na sehemu ya tano lazima itaongezwa kwenye thamani hiyo. Na kama mnyama hakombolewi, naye atauzwa kwa thamani iliyowekwa.
28Hakutakuwa na kitu amabacho mtu anakitoa kwa Yahweh, kutoka katika vyote alivyonavyo, iwe ni mwanadamu au mnyama, au ardhi ya familia yake, ambacho chaweza kuuzwa au kukombolewa. Kila kitu kitolewacho ni kitakatifu sana kwa Yahweh.
29Hakuna fidia inayoweza kulipwa kwa ajili ya mtu aliyetolewa ili kuangamizwa. Mtu huyo sharti auawe
30Zaka yote iliyo ya ardhini, iwe nafaka ichipukayo juu ya ardhi au tunda kutoka kwenye miti, ni mali ya Yahweh. Ni takatifu kwa Yahweh.

Read Mambo ya Walawi 27Mambo ya Walawi 27
Compare Mambo ya Walawi 27:1-30Mambo ya Walawi 27:1-30