Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 26

Mambo ya Walawi 26:26-38

Help us?
Click on verse(s) to share them!
26Nitakapokomesha mgao wa chakula, wanawake kumi wataweza kuoka mkate wako katika chombo kimoja cha kuokea na watakugawia mkate wako kwa uzani. Nanyi mtakula lakini hamtatoshelezwa.
27Endapo hamtanisikiliza pamoja na mambo haya kuwapata, lakini mkazidi kuenenda kinyume na mimi,
28kisha nami nitakwenda kinyume nanyi katika hasira, Nami nitawaadhibu hata mara saba kulingana na wingi wa dhambi zenu.
29Ndipo mtakapokula nyama ya wana wenu; mtakula nyama ya binti zenu.
30Nitapaangamiza mahali penu pa juu, kuziangusha chini madhabahu zenu za kufukizia uvumba, na kuzitupa maiti zenu juu ya maiti ya sanamu zenu, na Mimi mwenyewe nitawadharau nyinyi.
31Nitaigeuza miji yennu kuwa magofu na kupaharibu patakatifu penu. Nami sitapendezwa na harufu nzuri ya matoleo yenu.
32Nami nitaiharibu nchi. Adui zenu watakaokuwa wakiishi humo watashtushwa na uharibifu huo.
33Nami nitawatawanya nyinyi katika mataifa, na nitaufuta upanga wangu na kuwafuatia. Nchi yenu itatelekezwa, na miji yenu itakuwa magofu.
34Nayo nchi itazifurahia Sabato zake kwa kuwa itakuwa imetelekezwa na ninyi mkiwa katika nchi za daui zenu. Katika nyakati hizo, nchi itapumzika na kufurahia Sabato zake.
35Maadamu itakuwa imetelekezwa, itakuwa na pumziko, ambalo litakuwa ni pumziko iliyolikosa pamoja na Sabato zenu mlipokuwa mkiishi ndani yake.
36Na kwa wale watakoachwa humo kwenye nchi za adui zenu, Nitatuma hofu ndani ya mioyo yenu kiasi kwamba hata kama ni maelfu ya majani tu yatakapopeperushwa katika upepo yatawaogofyeni. Nanyi mtaanguka hata kama hakutakuwa na awafukuzaye.
37Mtajikwaa kila mmoja juu ya mwenzake kama vile mlikuwa mkiukimbia upanga, hata kama hakutakuwa na awafukuzaye nyinyi. Hamtakuwa na nguvu ya kusimama mbele ya daui zenu.
38Nanyi mtaangamia miongoni mwa mataifa, nayo nchi ya adui zenu yenyewe itawamezani.

Read Mambo ya Walawi 26Mambo ya Walawi 26
Compare Mambo ya Walawi 26:26-38Mambo ya Walawi 26:26-38