Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 26

Mambo ya Walawi 26:19-27

Help us?
Click on verse(s) to share them!
19Nami nitakivunja kiburi chenu katika uwezo wenu. Nitaifanya mbingu juu yenu iwe kama chuma na nchi yenu kama shaba.
20Nguvu yenu itatumika bure, kwa sababu nchi yenu haitazalisha mavuno yake, na miti yenu katika nchi haitazaa matunda yake.
21Iwapo mtataenenda kinyume changu na hamtanisikiliza mimi, nitaleta mapigo mara saba zaidi juu yenu, sawasawa na dhambi zenu.
22Nitatuma wanyama mapori hatari dhidi yenu, ambao watawaibia watoto wenu, kuangamiza mifugo yenu na kuwafanya mwe wachache katika idadi yenu. Hivyo barabara zenu zitakuwa nyeupe.
23Endapo pamoja na mambo haya kuwapata lakini msiyakubali marekebisho yangu na mkazidi kuenenda katika upinzani dhidi yangu,
24ndipo nami pia nitaenenda kinyume chenu, na Mimi mwenyewe nitawaadhibu mara saba kwa sababu ya dhambi zenu.
25Nitaleta upanga juu yenu utakaowaadhibu kwa kisasi kwa sababu ya kulivunja agano. Nanyi mtajikusanya kwenye miji yenu, Nami nitatuma humo maafa miongoni mwenu, na mtachukuliwa mikononi mwa adui yenu.
26Nitakapokomesha mgao wa chakula, wanawake kumi wataweza kuoka mkate wako katika chombo kimoja cha kuokea na watakugawia mkate wako kwa uzani. Nanyi mtakula lakini hamtatoshelezwa.
27Endapo hamtanisikiliza pamoja na mambo haya kuwapata, lakini mkazidi kuenenda kinyume na mimi,

Read Mambo ya Walawi 26Mambo ya Walawi 26
Compare Mambo ya Walawi 26:19-27Mambo ya Walawi 26:19-27