Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 25

Mambo ya Walawi 25:35-47

Help us?
Click on verse(s) to share them!
35Ikiwa mwananchi mwenzako anakuwa masikini, kiasi kwamba hawezi kujihudumia, nawe utalazimika kumsaidia kama vile ungemsaidia mgeni au mwingine yeyote kutoka nje aishie miongoni mwenu.
36Usimtoze riba au kujaribu kunufaika kutoka kwake katika njia yoyote, bali mheshimu Mungu wako ili kwamba ndugu yako aendelee kuishi nawe.
37Hutampa mkopo wa fedha na kumtoza riba, wala hutamuuzia chakula chako ili kupata faida.
38Mimi ndimi Yahweh Mungu wako, aliye kuleta wewe kutoka nchi ya Misri, ili kwamba Nikupe nchi ya Kanaani, na kwamba niwe Mungu wako.
39Iwapo mwananchi mwenzako atakuwa masikini na kujiuza mwenyewe kwako, hutamfanyisha kazi kama mtumwa.
40Mtendee kama mtumishi wa kuajiriwa. Ni lazima awe kama yule ahudumuye nawe kwa muda mpaka mwaka wa Yubile.
41Kisha ataondoka kwako, yeye mwenyewe na watoto wake pamoja naye, na atarejea kwenye familia yake mwenyewe na kwenye miliki ya baba yake.
42Kwa sababu wao ni watumishi wangu niliowaleta kutoka katika nchi ya Misri. Hawatauzwa kama watumwa.
43Usitawale juu yao kwa ukatili, bali yakupasa kumheshimu Mungu wako.
44Kwa upande wa watumwa wako wakiume na watumwa wako wa kike, unaowezao kuwapata kutok kwa mataifa yanayokuzunguka, waweza kununua watumwa kutoka kwao.
45Unaweza pia kununua watumwa kutoka kwa wageni wanaoishi miongoni mwenu, yaani, kutoka familia zao waliopamoja nawe, wale wtoto waliozaliwa katika nchi yako. Wanaweza kuwa mali yako.
46Unaweza kuzalisha watumwa hao kama urithi kwa watoto wako baada yako, ili kuwamiliki kama mali. Kutoka kwao waweza kununua watumwa daima, lakini hamtawezi kutawala kwa ukali juu ya ndugu zenu walio miogoni mwa watu wa Israeli.
47Iwapo mgeni anayeishi nawe kwa muda anakuwa tajiri, na ikiwa mmoja wa Waisraeli amekuwa masikini na kujuza mwenyewe kwa familia ya mgeni, au kwa mtu fulani katika familia,

Read Mambo ya Walawi 25Mambo ya Walawi 25
Compare Mambo ya Walawi 25:35-47Mambo ya Walawi 25:35-47