Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 25

Mambo ya Walawi 25:3-9

Help us?
Click on verse(s) to share them!
3Ni lazima mtapanda mazao yenu kwa miaka sita, na kwa miaka sita mtaikatia matawi mizabibu yenu na kukusanya mazao yake.
4Lakini katika mwaka wa saba, Sabato ya pumziko la utulivu kwa nchi itashikwa, ni Sabato kwa Yahweh. Hamtapanda mashamba yenu wala kuikatia mizabibu yenu matawi yake.
5Hamtasimamia mavuno yoyote ya mazao ya mizabibu iliyojiotesha yenyewe katika mashamba yenu ya mizabibu isiyokatiwa matawi. Huu utakuwa mwaka wa pumziko lenye utulivu kwa ardhi.
6Chochote ardhi isiyofanyiwa kazi itakachotoa wakati wa Sabato ndicho kitakuwa chakula chako. Wewe mwenyewe, watumwa wako wa kiume na wa kike, watumishi wako wa kuajiriwa na wageni wanaoishi pamoja nawe mnaweza kujikusanyia chakula.
7Na wnyama wako wa kufugwa na wanyama pori waweze kula chochote ardhi itoacho.
8Ni lazima kwenu kuhesabu Sabato saba za miaka, yaani, saba mara miaka saba, ikifanya jumla ya miaka arobaini na tisa.
9Kisha mtapiga sauti ya tarumbeta kila mahali katika siku ya kumi ya mwezi wa saba. Katika Siku ya Upatanisho ni lazima mtapiga tarumbeta katika nchi yenu yote.

Read Mambo ya Walawi 25Mambo ya Walawi 25
Compare Mambo ya Walawi 25:3-9Mambo ya Walawi 25:3-9