Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 25

Mambo ya Walawi 25:21-33

Help us?
Click on verse(s) to share them!
21Nitaiamru baraaka yangu ije juu yenu katika mwaka wa sita, nayo itatoa mavuno ya kutosha kwa miaka mitatu.
22Mtapanda katika mwaka wa nane na mtaendelea kula mazao ya miaka iliyopita na kutoka kwenye ghala la chakula. Mpaka mavuno ya mwaka wa tisa yatakapofika, mtaweza kula kutoka kwenye riziki iliyohifadhiwa katika miaka iliyopita
23Ardhi haitauzwa kwa mmiliki mpya wa kudumu, kwa sababu ardhi ni mali yangu. Ninyi nyote mu wageni na wakazi wa muda juu ya ardhi yangu.
24Ni lazima muitunze haki ya ukombozi kwa ajili ya ardhi yote mtakayoimiliki; itawapasa kuruhusu ardhi inunuliwe tena na familia ambayo wewe uliinunua hiyo ardhi kutoka kwao.
25Iwapo Mwisraeli mwenzako anakuwa masikini na kwa sababu hiyo anauza baadhi ya miliki yake, kisha jamaa yake wa karibu anaweza kuja na kuikomboa hiyo miliki ambayo jamaa yake kaiuza kwako.
26Iwapo mtu hana jamaa wa kuikomboa mali yake, lakini ikiwa kafanikiwa na anao uwezo wa kuikomboa,
27kisha atahesabu miaka tangu ardhi hiyo ilipouzwa na kurejesha kwa mtu aliyemuuzia fedha iliyosalia. Naye anaweza kuerejea kwenye miliki yake mwenyewe.
28Lakini ikiwa hawezi kuirejesha kwake ardhi aliyoiuza, nayo hiyo ardhi aliyoiuza itabaki katika umiliki wa yule aliyeinunua mpaka mwaka wa Yubile. Kwenye mwaka wa Yubile, ardhi itarejeshwa kwa mtu aliyeiuza, naye mmiliki wa asili atarejea kwenye mali yake.
29Ikiwa mtu anauza nyumba iliyo kwenye mji uliozungushiwa ukuta, naye anaweza kuinunua tena ndani ya mwaka baada ya kuuzwa. kwa kuwa, kwa mwaka mzima atakuwa na haki ya ukombozi.
30Kama nyumba hiyo haitakombolewa kabla ya mwaka mzima, ndipo hiyo nyumba iliyoko kwenye mji uliozungushiwa ukuta itakuwa mali ya kudumu ya yule aliyeinunua, katika vizazi vyote vya uzao wake. Nyumba hiyo haitakuwa ya kurejeshwa katika mwaka wa Yubile.
31Lakini nyumba za vijijini zisizokuwa na ukuta kuzizunguuka, zitahesabiwa kuwa shamba la nchi. Zaweza kukombolewa, na ni lazima zirejeshwe katika mwaka wa Yubile.
32Hata hivyo, nyumba zinazomilikiwa na makuhani katika miji yao zaweza kukombelewa wakati wowote.
33Iwapo mmoja wa makuhani haikombowi nyumba iliyozwa, kisha nyumba hiyo iliyouzwa katika miji ilimo, ni lazima irejeshwe katika mwaka wa Yubile, kwa kuwa nyumba za miji ya makuhani ni mali yao miongoni mwa watu wa Israeli.

Read Mambo ya Walawi 25Mambo ya Walawi 25
Compare Mambo ya Walawi 25:21-33Mambo ya Walawi 25:21-33