Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 25

Mambo ya Walawi 25:10-42

Help us?
Click on verse(s) to share them!
10Nanyi mtautenga mwaka wa hamsini kwa ajili ya Yahweh na mtatangaza uhuru katika nchi yote kwa wakazi wote. Kutakuwa na Yubile kwa ajili yenu, ambayo kwayo mali na watumwa ni lazima warejeshwe kwa familia zao.
11Mwaka wa saba kutakuwa na Yubile kwenu. Hamtapanda wala kusimamia mavuno ya kijioteshacho chenyewe, na kukusanya kichipukacho kwenye mizabibu isiyokatiwa matawi.
12Kwa sababu hiyo ni Yubile takatifu kwenu. Nanyi mtakula mazao yanayokua yenyewe kutoka mashambani.
13Ni lazima muwarejeshe kila mmoja kwenye miliki yake katika mwaka huu wa Yubile.
14Iwapo utauza ardhi yoyote ya jirani yako au kununua ardhi yake, ni shrti msipunjane au kutendeana kwa hila.
15Iwapo unanunua ardhi kutoka kwa jirani yako, zingatia idadi ya miaka na mazao ambayo yaweza kuvunwa mpaka mwaka wa Yubile nyingine. Jirani yako anayeuza ardhi ni lazima aihesabu miaka hiyo pia.
16Miaka inapoongezeka mpaka Yubile nyingine, ataongeza thamani ya ardhi, na miaka inapokuwa michache kufikia Yubile nyingine atashusha thamani, kwa sababu idadi ya mavuno inahusiana na idadi ya miaka kabla ya Yubile nyingine.
17Msipunjane au kutendeana kwa hila, badala yake, yawapasa kumheshi Yahweh Mungu wenu.
18Kwa hiyo basi, ni lazima muyatii maagiza, kuzitunza sheria zangu na kuzitekeleza. Nanyi mtaishi katika nchi katika usalama.
19Nayo nchi itawapa mavuno yake, nanyi mtakula matunda yenu na mtaishi humo salama.
20Labda mtasema, Tutakula nini katika mwaka wa saba? Tazama, hatuwezi kupanda wala kukusanya mazao yetu.”
21Nitaiamru baraaka yangu ije juu yenu katika mwaka wa sita, nayo itatoa mavuno ya kutosha kwa miaka mitatu.
22Mtapanda katika mwaka wa nane na mtaendelea kula mazao ya miaka iliyopita na kutoka kwenye ghala la chakula. Mpaka mavuno ya mwaka wa tisa yatakapofika, mtaweza kula kutoka kwenye riziki iliyohifadhiwa katika miaka iliyopita
23Ardhi haitauzwa kwa mmiliki mpya wa kudumu, kwa sababu ardhi ni mali yangu. Ninyi nyote mu wageni na wakazi wa muda juu ya ardhi yangu.
24Ni lazima muitunze haki ya ukombozi kwa ajili ya ardhi yote mtakayoimiliki; itawapasa kuruhusu ardhi inunuliwe tena na familia ambayo wewe uliinunua hiyo ardhi kutoka kwao.
25Iwapo Mwisraeli mwenzako anakuwa masikini na kwa sababu hiyo anauza baadhi ya miliki yake, kisha jamaa yake wa karibu anaweza kuja na kuikomboa hiyo miliki ambayo jamaa yake kaiuza kwako.
26Iwapo mtu hana jamaa wa kuikomboa mali yake, lakini ikiwa kafanikiwa na anao uwezo wa kuikomboa,
27kisha atahesabu miaka tangu ardhi hiyo ilipouzwa na kurejesha kwa mtu aliyemuuzia fedha iliyosalia. Naye anaweza kuerejea kwenye miliki yake mwenyewe.
28Lakini ikiwa hawezi kuirejesha kwake ardhi aliyoiuza, nayo hiyo ardhi aliyoiuza itabaki katika umiliki wa yule aliyeinunua mpaka mwaka wa Yubile. Kwenye mwaka wa Yubile, ardhi itarejeshwa kwa mtu aliyeiuza, naye mmiliki wa asili atarejea kwenye mali yake.
29Ikiwa mtu anauza nyumba iliyo kwenye mji uliozungushiwa ukuta, naye anaweza kuinunua tena ndani ya mwaka baada ya kuuzwa. kwa kuwa, kwa mwaka mzima atakuwa na haki ya ukombozi.
30Kama nyumba hiyo haitakombolewa kabla ya mwaka mzima, ndipo hiyo nyumba iliyoko kwenye mji uliozungushiwa ukuta itakuwa mali ya kudumu ya yule aliyeinunua, katika vizazi vyote vya uzao wake. Nyumba hiyo haitakuwa ya kurejeshwa katika mwaka wa Yubile.
31Lakini nyumba za vijijini zisizokuwa na ukuta kuzizunguuka, zitahesabiwa kuwa shamba la nchi. Zaweza kukombolewa, na ni lazima zirejeshwe katika mwaka wa Yubile.
32Hata hivyo, nyumba zinazomilikiwa na makuhani katika miji yao zaweza kukombelewa wakati wowote.
33Iwapo mmoja wa makuhani haikombowi nyumba iliyozwa, kisha nyumba hiyo iliyouzwa katika miji ilimo, ni lazima irejeshwe katika mwaka wa Yubile, kwa kuwa nyumba za miji ya makuhani ni mali yao miongoni mwa watu wa Israeli.
34Lakini yale mashamba yanayozunguka miji yao hayataweza kuuzwa kwa sababu hiyo ni mali ya kudumu ya Makuhani.
35Ikiwa mwananchi mwenzako anakuwa masikini, kiasi kwamba hawezi kujihudumia, nawe utalazimika kumsaidia kama vile ungemsaidia mgeni au mwingine yeyote kutoka nje aishie miongoni mwenu.
36Usimtoze riba au kujaribu kunufaika kutoka kwake katika njia yoyote, bali mheshimu Mungu wako ili kwamba ndugu yako aendelee kuishi nawe.
37Hutampa mkopo wa fedha na kumtoza riba, wala hutamuuzia chakula chako ili kupata faida.
38Mimi ndimi Yahweh Mungu wako, aliye kuleta wewe kutoka nchi ya Misri, ili kwamba Nikupe nchi ya Kanaani, na kwamba niwe Mungu wako.
39Iwapo mwananchi mwenzako atakuwa masikini na kujiuza mwenyewe kwako, hutamfanyisha kazi kama mtumwa.
40Mtendee kama mtumishi wa kuajiriwa. Ni lazima awe kama yule ahudumuye nawe kwa muda mpaka mwaka wa Yubile.
41Kisha ataondoka kwako, yeye mwenyewe na watoto wake pamoja naye, na atarejea kwenye familia yake mwenyewe na kwenye miliki ya baba yake.
42Kwa sababu wao ni watumishi wangu niliowaleta kutoka katika nchi ya Misri. Hawatauzwa kama watumwa.

Read Mambo ya Walawi 25Mambo ya Walawi 25
Compare Mambo ya Walawi 25:10-42Mambo ya Walawi 25:10-42