Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 23

Mambo ya Walawi 23:2-42

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2“Zungumza na watu wa Israeli, na uwaambie, 'Hizi ndizo sikukuu zilizoamriwa kwa ajili ya Yahweh, ambazo ni lazima mzitangaze kuwa makusanyiko matakatifu, ni sikukuu zangu za mara kwa mara.
3Mnaweza kufanya kazi kwa siku sita, lakini siku ya saba ni Sabato ya kupumzika kabisa. Usifanye kazi kwa sababu ni Sabato kwa ajili ya Yahweh mahali pote mnaposhi.
4Hizi ndizo sikukuu za Yahweh zilizoamriwa, Makusanyiko matakatifu mtakayoyatangaza kwa nyakati zilioamriwa:
5Katika mwenzi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi kwenye mwanga hafifu wa machweo ya jua, ni Pasaka ya Yahweh.
6Siku ya kumi na tano ya mwezi ule ule ni sikukuu ya mikate isiotiwa hamira kwa ajili ya Yahweh. Kwa muda wa siku saba mtakula mikate isiotiwa hamira.
7Siku ya kwanza ni lazima mjitenge kwa pamoja, hamtafanya kazi ya kawaida.
8Kwa siku saba mtamletea Yahweh matoleo ya chakula. Siku ya saba ni ya kusanyiko takatifu lililotengwa kwa ajili ya Yahweh, nanyi katika siku hiyo hamtafanya kazi yoyote ya kawaida.”
9Yahweh akamwambia Musa, akisema,
10“Sema na watu wa Israeli uwaambie, 'mtakapika kwenye nchi nitakayowapa nyinyi, na mtakapovuna mazao yake, nanyi yawapasa kumletea kuhani fungu la masuke ya nafaka ya matunda yake ya kwanza.
11Naye ataliinua hilo fungu la masuke ya nafaka mbele za Yahweh na kulileta kwake, kwa kuwa litakubalika kwa niaba yenu. Nalo litaletwa siku baada ya Sabato ili kwamba kuhani ataliinua na kulileta kwangu.
12Siku ile mtakapoliinua lile fungu la masuke ya nafaka na kulileta kwangu, itawabidi kutoa mwana—kondoo dume wa mwaka mmoja na asiye na dosari awe sadaka ya kuteketezwa kwa Yahweh.
13Matoleo ya nafaka yatakuwa sehemu za kumi za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta, uwe matoleo yaliyofanywa kwa moto kwa Yahweh, ili kutoa harufu nzuri ya kupendeza, pamoja na hiyo kutakuwa na matoleo ya kinywaji ya divai, moja ya nne ya hini.
14Hamtakula mkate, wala nafaka iliyokaangwa au nafaka mpya hata siku ile mliyoleta matoleo haya kwa Mungu wenu. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu, popote pale mnapoishi.
15Tangu siku iliyofuata baada ya Sabato—hiyo ilikuwa siku mlipolileta lie fungu la nafaka la matoleo ya kutikiswa—hesabuni majuma saba kamili.
16Mtahesabu siku hamsini, ambazo zingekuwa siku baada ya Sabato ya saba. Kisha mtaleta matoleo ya nafaka mpya kwa Yahweh.
17Mtaleta kutoka nyumbani mwenu mikate miwili iliyotengenezwa kutokana na mbili za kumi za efa. Ni lazima ifanywe kwa unga laini na uliochanganywa na hamira; zitakuwa matoleo ya kutikiswa ya malimbuko ya kwanza kwa Yahweh.
18Mtaileta hiyo mikate pamoja na wana—kondoo saba wa mwaka mmoja na wasiokuwa na dosari, fahali mmoja mchanga na dume wa kondoo wawili. Watakuwa matoleo ya kuteketezwa kwa moto kwa Yahweh, pamoja na matoleo yao ya nafaka na matoleo ya kinywaji, matoleo yaliyofanywa kwa moto na kutoa harufu nzuri ya kupendeza kwa Yahweh.
19Ni lazima mtowe mbuzi dume mmoja kwa ajili ya matoleo ya dhambi, na wana—kondoo dume wawili wa mwaka mmoja kwa ajili ya dhabihu, wawe matoleo ya ushirika.
20Ni lazima kuhani azitikise pamoja na mkate wa malimbuko ya kwanza mbele za Yahweh na kuzileta kwake kuwa matoleo pamoja na kondoo dume wawili. Watakuwa sadaka takatifu kwa Yahweh kwa ajili ya kuhani.
21Mtatoa tangazo siku iyo hiyo. Kutakuwa na kusanyiko takatifu, na hamtafanya kazi za kawaida. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vya watu wenu mahali pote mnapoishi.
22Mtakapovuna mazao ya nchi yenu, Msivune kabisa kabisa pembeni mwa mashamba yenu, wala msivune mazazo ya mavuno yenu. Inawapasa kuyaacha kwa ajili ya masikini na mgeni. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.”
23Yahweh akazungumza na Musa, akisema,
24“Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, “Siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza itakuwa siku ya pumzika makini kwa ajili yenu, kumbukumbu pamoja na kupigwa kwa tarumbeta na kusanyiko takatifu,
25Hamtafanya kazi ya kawaida, na ni lazima mtoe dhabihu inayofanywa kwa moto kwa Yahweh.”
26Kisha Yahweh akamwambia Musa, akisema,
27“Sasa, siku ya kumi ya mwezi huu wa saba, ni Siku ya Upatanisho. Kutakuwa na kusanyiko takatifu, na ni lazima mjinyenyekeze na kuleta kwa Yahweh matoleo kwa moto.
28Hamtafanya kazi katika siku hiyo kwa sababu ni Siku ya Upatanisho, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu mbele za Yahweh Mungu wenu.
29Yeyote asiyejinyenyekeza siku hiyo lazima akatiliwe mbali na watu wake.
30Yeye afanyaye kazi yoyote katika siku hiyo, Mimi, Yahweh, nitamwangamiza atoke miongoni mwa watu wake.
31Msifanye kazi ya aina yoyote katika siku hiyo. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu mahali pote mnapoishi.
32Siku hii itakuwa Sabato ya pumziko lenye utlivu, na ni lzima siku ya tisa ya mwezi mjinyenyekeze katika majira ya jioni. Tangu jioni hata jioni mtaishika Sabato yenu.”
33Yahweh akazungumza na Musa, akisema,
34“Zungumza na watu ISraeli, uwaambie 'Katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba kutakuwa na Sikukuu ya vibanda kwa Yahweh. nayo itadumu siku saba.
35Siku ya kwanza kutakuwa na kusanyiko takatifu. Hamtafanya kazi ya kawaida.
36Kwa muda wa siku saba mtatoa dhabihu iliyofanywa kwa moto kwa Yahweh. Siku ya nane kutakuwa na kusanyiko takatifu, nanyi mtato dhabihu iliyofanywa kwa moto kwa Yahweh. Hili ni kusanyiko lenye utulivu, nanyi msifanye kazi yoyote ya kawaida.
37Hizi ndizo sikukuu zilizoamriwa kwa ajili ya Yahweh, ambazo mnapaswa kuzitangaza kuwa ni makusanyiko matakatifu ya kutoa dhabihu kwa moto kwa Yahweh, matoleo ya kuteketezwa na matoleo ya nafaka, dhabihu na matoleo ya vinywaji, kila moja kwa siku yake.
38Sikukuu hizi zitakuwa nyongeza kwa Sabato za Yahweh na zawadi zenu, viapo vyenu vyote, na sadaka zenu zote za hiari mzitoazo kwa Yahweh.
39Kuhusu Sikukuu ya vibanda, siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, mtakapokuwa mmeyakusanya ndani matunda ya nchi, ni lazima muitunze sikukuu hii ya Yehweh kwa muda wa siku saba. Siku ya kwanza itakuwa ya pumziko lenye utulivu, na siku ya nane pia itakuwa ya pumziko lenye utulivu.
40Siku ya kwanza mtachuma tunda lililobora kutoka kwenye miti, mtakata makuti ya mtende, na matawi ya miti minene yenye majani mengi, na majani ya mierebi kutoka chemchemi za maji, nanyi mtashangilia mbele za Yahweh Mungu wenu kwa siku saba.
41Kwa muda wa siku saba kila mwaka, mtaisherehekea sikukuu hii kwa Yahweh. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu mahali potepote mtakapoishi. Mtaisherehekea sikukuu hii katika mwezi wa saba.
42Mtaishi kwenye vibanda vidogovidogo kwa siku saba. Waisraeli wenyeji wa kuzaliwa wote itawapasa kuishi katika vibanda vidogovidogo kwa siku saba,

Read Mambo ya Walawi 23Mambo ya Walawi 23
Compare Mambo ya Walawi 23:2-42Mambo ya Walawi 23:2-42