Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 23

Mambo ya Walawi 23:12-20

Help us?
Click on verse(s) to share them!
12Siku ile mtakapoliinua lile fungu la masuke ya nafaka na kulileta kwangu, itawabidi kutoa mwana—kondoo dume wa mwaka mmoja na asiye na dosari awe sadaka ya kuteketezwa kwa Yahweh.
13Matoleo ya nafaka yatakuwa sehemu za kumi za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta, uwe matoleo yaliyofanywa kwa moto kwa Yahweh, ili kutoa harufu nzuri ya kupendeza, pamoja na hiyo kutakuwa na matoleo ya kinywaji ya divai, moja ya nne ya hini.
14Hamtakula mkate, wala nafaka iliyokaangwa au nafaka mpya hata siku ile mliyoleta matoleo haya kwa Mungu wenu. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu, popote pale mnapoishi.
15Tangu siku iliyofuata baada ya Sabato—hiyo ilikuwa siku mlipolileta lie fungu la nafaka la matoleo ya kutikiswa—hesabuni majuma saba kamili.
16Mtahesabu siku hamsini, ambazo zingekuwa siku baada ya Sabato ya saba. Kisha mtaleta matoleo ya nafaka mpya kwa Yahweh.
17Mtaleta kutoka nyumbani mwenu mikate miwili iliyotengenezwa kutokana na mbili za kumi za efa. Ni lazima ifanywe kwa unga laini na uliochanganywa na hamira; zitakuwa matoleo ya kutikiswa ya malimbuko ya kwanza kwa Yahweh.
18Mtaileta hiyo mikate pamoja na wana—kondoo saba wa mwaka mmoja na wasiokuwa na dosari, fahali mmoja mchanga na dume wa kondoo wawili. Watakuwa matoleo ya kuteketezwa kwa moto kwa Yahweh, pamoja na matoleo yao ya nafaka na matoleo ya kinywaji, matoleo yaliyofanywa kwa moto na kutoa harufu nzuri ya kupendeza kwa Yahweh.
19Ni lazima mtowe mbuzi dume mmoja kwa ajili ya matoleo ya dhambi, na wana—kondoo dume wawili wa mwaka mmoja kwa ajili ya dhabihu, wawe matoleo ya ushirika.
20Ni lazima kuhani azitikise pamoja na mkate wa malimbuko ya kwanza mbele za Yahweh na kuzileta kwake kuwa matoleo pamoja na kondoo dume wawili. Watakuwa sadaka takatifu kwa Yahweh kwa ajili ya kuhani.

Read Mambo ya Walawi 23Mambo ya Walawi 23
Compare Mambo ya Walawi 23:12-20Mambo ya Walawi 23:12-20