Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 22

Mambo ya Walawi 22:25-30

Help us?
Click on verse(s) to share them!
25Usifanye haya katika nchi yako. Usilete mkate wa Mungu wako kutoka mkononi mwa mgeni. Hao wanyama wenye vilema na dosari ndani yao, hawatapokelewa kabisa kwa ajili yako.
26Yahweh akamwambia Musa na akasema,
27“Wakati ndama, mwana—kondo au mwana—mbuzi azaliwapo, sharti abaki na mama yake kwa muda wa siku saba. Ndipo kuanzia siku ya nane na kuendelea, anaweza kupokelewa kuwa dhabihu iliyofanywa kwa moto kwa Yahweh.
28Usimchinje ng'ombe jike pamoja na ndama wake au mbuzi jike pamoja na kitoto chake kwa siku moja.
29Utoapo sadaka ya shukrani kwa Yahweh utaitoa kwa njia iliyokubalika.
30Ni lazima iliwe siku iyo hiyo inayotolewa. Hutakiwi kubakiza chochote hata asubuhi. Mimi ndimi Yahweh.

Read Mambo ya Walawi 22Mambo ya Walawi 22
Compare Mambo ya Walawi 22:25-30Mambo ya Walawi 22:25-30