Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 22

Mambo ya Walawi 22:1-13

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Yahweh akazungumza na Musa, kusema,
2“Ongea na Aroni na wanawe, waambie wajiepushe na vitu vitakatifu vya watu wa Israeli wanavyovitenga kwangu. Wasilinajisi jina langu. Mimi ndimi Yahweh.
3Waambie, 'Ikiwa mmoja wa wazao wenu katika vizazi vyenu vyote anakaribia vitu vitakatiifu vile ambavyo watu wa Israeli wamevitenga kwa Yahweh, wakati akiwa najisi, sharti mtu huyo akatiliwe mbali atoke mbele zangu. Mimi ndimi Yahweh.
4Hatakuwapo yeyote wa uzao wa Aroni aliye na ungonjwa wa ngozi wa kuambukiza, au maambukizi yatirirkayo kutoka mwilini mwake, atakayekula sehemu yoyote ya dhabihu inatolewayo kwa Yahweh mpaka atakapotakasika. Yeyote agusaye kitu chochote kilichonajisi kwa njia ya kugusa maiti, au kwa kumgusa mtu yeyote aliyetokwa na shahawa,
5au yeyote agusaye mnyama atakayemtia unajisi, au mtu yeyote atakayemfanya najisi, kwa hiyo unajisi wowote unaweza kuwa—
6kuhani yeyote agusaye kitu chochote kisichosafi atakuwa najisi hata jioni. Hatakula chochote cha vitu vitakatifu, isipokuwa ameuosha mwili wake katika maji.
7Jua linapotua, ndipo atakuwa safi. Baada ya machweo anaweza kula kutoka katika vitu vitakatifu, kwasababu hivyo ni vyakuala vyake.
8Asile mzoga wowote uliookotwa au mnyama aliyeraruliwa na wanyama pori, ambaye kwake atajitia unajisi. Mimi ndimi Yahweh.
9Ni lazima makuhani wafuate maagizo yangu, ama sivyo watakuwa na hatia ya dhambi na wangeweza kufa kwa kunitia unajisi. Mimi ndimi Yahweh ninayewafanya wao watakatifu.
10Hakuna mtu kutoka nje ya familia ya kuahani, wakiwemo wageni wa kuhani au watumwa wake wa kuajiliwa, atakayeweza kula kitu chochote kilicho kitakatifu.
11Lakini kama huyo kuhani amenunua mtumwa kwa fedha yake mwenyewe, mtumwa huyo anaweza kula kutoka katika vitu vilivyotengwa kwa Yahweh. Na watu wa familia ya kuhani na watumwa waliozaliwa nyumbani mwake, pia wanaweza kula pamoja naye kutoka katika vitu hivyo.
12Ikiwa binti wa kuhani ameolewa na mtu asiye kuhani, hataweza kula chochote cha mchango wa matoleo matakatifu.
13Lakini ikiwa huyo binti wa kuhani ni mjane au ametalikiwa, na ikiwa hana mtoto, na anarudi kuishi knyumbani kwa baba yake kama alivyokuwa wakati wa ujana wake, anaweza kula kutoka katika chakula cha baba yake. Lakini hakuna yeyote asiye wa familia ya kikuhani anatakayeruhusiwa kula kutoka katika chakula cha kuhani.

Read Mambo ya Walawi 22Mambo ya Walawi 22
Compare Mambo ya Walawi 22:1-13Mambo ya Walawi 22:1-13