Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 21

Mambo ya Walawi 21:1-9

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Yahweh akamwambia Musa, “Zungumza na makuhani, wana wa Aroni, nawe waambie, 'hakuna hata mmoja miongoni mwenu atakayejitia unajisi kwa wale wanaokufa miongoni mwa watu wake,
2isipokuwa yule aliye ndugu wa karibu—mama yake, baba yake, mwanawe, bintiye, nduguye,
3au dada yake bikira anayemtegemea, kwa kuwa hana mume—kwake huyo anaweza kujitia unajisi.
4Lakini hatajitia unajisi na kujichafu kwa ajili ya jamaa wengine.
5Makuhanai hawatanyoa vichwa vyo wala kunyoa pembeni mwa ndevu zao, wala hawatachanja chale miili yao.
6Watakuwa watakatifu kwa Mungu wao, wala hawataliaibisha jina la Mungu wao, kwa sababu makuhani hutoa sadaka ya Yahweh ya chakula, mkate wa Mungu wao. Kwa hiyo makuhani lazima wawe watakatifu.
7Hawataoa mwanamke aliye kahaba na aliyetiwa unajisi, na hawataoa mwanamke aliyetalikiwa kutoka kwa mume wake kwa sababu wametengwa kwa ajili ya Mungu wao.
8Utamtenga kwa sababu yeye ndiye anayetoa mkate kwa Mungu wako. Ni lazima awe mtakatifu, kwa sababu—Mimi, Yahweh, ndimi niwatakasaye nyinyi—pia Mimi mwenyewe ni mtakatifu.
9Binti yeyote wa kuhani anayejitia unajisi kwa kujifanya kahaba anajifedhehesha mwenyewe. Ni lazima ateketezwe kwa moto.

Read Mambo ya Walawi 21Mambo ya Walawi 21
Compare Mambo ya Walawi 21:1-9Mambo ya Walawi 21:1-9