Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 20

Mambo ya Walawi 20:2-9

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2“Waambie watu wa Waisraeli, 'mtu yeyote miongoni mwa watu Israeli, au Mgeni yeyote anayeishi miongoni mwa Waisraeli atakayemtoa mtoto wake yeyote kwa Moleki, hakika atauawa. Ni lazima watu wa nchi wamponde kwa mawe.
3Pia nitaukaza uso wangu dhidi ya mtu huyo na kumkatilia mbali kutoka miongoni mwa watu wake kwa sababu amemtoa mtoto wake kwa Moleki, ili kupatia unajisi mahali pangu patakatifu na kulinajisi jina langu takatifu.
4Na kama watu wa nchi watayafumba macho yao kwa mtu huyo anapomtoa mmoja wa watoto wake kwa Moleki, kama hawatamwua mtu huyo, ndipo Mimi mwenyewe nitaukaza uso wangu dhidi ya mtu huyo na ukoo wake,
5Nami nitamkatilia mbali pamoja na yeyote anayejifanya kahaba ili kufanya umalaya na Moleki.
6Mtu yule anayewageukia wanaozungumza na wafu, au na wale wanaozungumza na roho ili kufanya ukahaba nao, Nitakaza uso wangu dhidi ya mtu huyo; Nami nitamkatilia mbali atoke miongoni mwa watu wake.
7Kwa hiyo jitakaseni wenyewe na muwe watakatifu, kwa sababu Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
8Mtazitunza amari zangu na kuzifuta. Mimi ndimi Yahweh anayewatenga ninyi muwe watakatifu.
9Yeyote amlaaniye baba yake au mama yake hakika mtu huyo atauawa. Amemlaani baba yake au mama yake, kwa hiyo ana hatia na anastahili kufa.

Read Mambo ya Walawi 20Mambo ya Walawi 20
Compare Mambo ya Walawi 20:2-9Mambo ya Walawi 20:2-9