Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 19

Mambo ya Walawi 19:2-12

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2Zungumza na kusanyiko lote la watu wa Israeli na uwaambie, 'Ni lazima muwe watakatifu, kwa kuwa mimi Yahweh Mungu wenu ni mtakatifu.
3Kila mtu amstahi mama yake na baba yake. Na ni lazima muzishike Sabato zangu. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
4Msizigeukie sanamu zisizo na thamani, wala kujitengenezea wenyewe miungu kutokana na chuma. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
5Unapotoa dhabihu za sadaka ya ushirika kwa Yahweh, utatoa ili kupata kibali.
6Ni sharti iliwe siku hiyo hiyo uliyoitoa, au siku inayofuata.
7Kama kinabaki kitu cho chote hata siku ya tatu ni lazima kiteketezwe kwa moto. Kama kitaliwa katika siku ya tatu kitakuwa najisi. Hakitakubalika,
8lakini kila akilaye ni lazima atachukua hatia yake kwa sababu amekivunjia heshima kilicho kitakatifu kwa Yahweh. Mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.
9Unapovuna mavuno ya ardhi yako, usivune hata pembezo mwa shamba lako kabisa, wala hutakusanya mabaki ya mavuno yako yote.
10Usikusanye kila zabibu kutoka katika mizabibu yako, wala usiziokote dhabibu zilizoanguka chini katika shamba la mizabibu. Ni lazima uziache kwa ajili ya masikini na kwa ajili ya wageni. Mimi ndimi Yahweh Mungu wako.
11Usiibe. Usiseme uongo. Msidanganyane.
12Usiape kwa jina langu kwa uongo na kulinajisi jina la Mungu wako. Mimi ndimi Yahweh

Read Mambo ya Walawi 19Mambo ya Walawi 19
Compare Mambo ya Walawi 19:2-12Mambo ya Walawi 19:2-12