Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 15

Mambo ya Walawi 15:9-22

Help us?
Click on verse(s) to share them!
9Tandiko lolote ambalo ambaye anamajimaji ya kisonono atalikalia litakuwa najisi.
10Yeyote anayegusa kitu chochote kilichokuwa chini ya mtu huyo atakuwa najisi mpaka jioni, na yeyote anayebeba vitu hivyo lazima afue nguo zake na aoge katika maji; atanajisika mpaka jioni.
11Ambaye anamajimaji kama hayo akimgusa kabla kwanza ya kuosha kwa maji safi mikono yake, mtu aliyeguswa lazima afue nguo zake na aoge katika maji, na atakuwa najisi mpaka jioni.
12Chungu chochote cha udongo ambacho ambaye anamajimaji kama hayo akigusa lazima kivunjwe, na kila chombo cha mti lazima kioshwe na maji safi.
13Wakati mwenye kisonono anapotakaswa katika kisonono chake, ndipo lazima ahesabu kwaajili yake siku saba kwaajili ya kutakasika kwake; ndipo afue nguo na aoshe mwili wake kwenye maji yatiririkayo. Ndipo atakuwa safi.
14Katika siku ya nane lazima achukue njiwa wawili au kinda mbili za njiwa na aje mbele za Yahwe pakuingilia kwenye hema ya mkutano; pale lazima atoe hao ndege kwa kuhani.
15Lazima kuhani awatoe, moja kama sadaka ya dhambi na nyingine kama ya kuteketezwa, na kuhani lazima afanye upatanisho kwaajili yake mbele za Yahwe kwaajili ya kisonono chake.
16Kama mtu yeyote ametokwa na shahawa, ndipo lazima aoge mwili wake wote katika maji; atanajisika mpaka jioni.
17Kila vazi au ngozi ambayo juu yake kuna shahawa lazama paoshwe kwa maji; itakuwa najisi mpaka jioni.
18Na kama mwanamke na mwanaume watalala pamoja na kunakutokwa kwa shahawa kwenda kwa mwanamke, lazima wote wawili waoge katika maji; watakuwa najisi mpaka jioni.
19Mwanamke anapokuwa kwenye hedhi, ataendelea kunajisika kwa siku saba, na yeyote anayemgusa atakuwa najisi mpaka jioni.
20Chochote anacholala juu yake wakati wa hedhi kitakuwa najisi; kila kitu ambacho anakalia kitakuwa pia najisi.
21Yeyote anayegusa kitanda chake lazima afue nguo zake na aoge kwa maji; mtu huyo atakuwa najisi mpaka jioni.
22Yeyote anayegusa chochote ambacho amekikalia lazima afue nguo zake na aoge kwa maji; mtu huyo anakuwa najisi mpaka jioni.

Read Mambo ya Walawi 15Mambo ya Walawi 15
Compare Mambo ya Walawi 15:9-22Mambo ya Walawi 15:9-22