22Yeyote anayegusa chochote ambacho amekikalia lazima afue nguo zake na aoge kwa maji; mtu huyo anakuwa najisi mpaka jioni.
23Iwe juu ya kitanda au kitu chochote juu ya popote atakapokaa, kama akikigusa, mtu huyo atakuwa najisi mpaka jioni.
24Kama mwanaume yeyote akilala naye, na unajisi wa mwanamke ukamgusa, atakuwa amenajisika siku saba. Kila kitanda ambacho anakilalia mwanaume huyo kitanajisika.
25Kama mwanamke ametokwa damu kwa siku nyingi ambayo siyo kipindi cha hedhi yake, au ikitoka zaidi ya kipindi chake cha hedhi, wakati wote wa siku za kunajisika, atakuwa kama alikuwa kwenye siku zake za hedhi. Yeye ni najisi.