Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 14

Mambo ya Walawi 14:14-40

Help us?
Click on verse(s) to share them!
14Kuhani atachukua baadhi ya damu ya sadaka ya hatia na kuiweka kwenye ncha ya sikio la kulia la mtu yule wa kutakaswa, katika dole gumba la kulia, katika dole la mguu wa kulia.
15Ndipo kuhani atachukua mafuta kutoka chombo na kuyamimina katika kiganja cha mkono wake wa kushoto, na kuzamisha kidole chake katika mafuta hayo yaliyo kwenye mkono wa kushoto,
16na kunyunyiza baadhi ya mafuta kwa kidole mara saba mbele za Yahwe.
17kuhani ataweka mafuta yaliyobaki kwenye mkono wake kwenye ncha ya sikio la kulia la mtu wa kutakaswa, juu ya dole gumba la mkono wa kulia, na katika dole kubwa la mguu wa kulia. Lazima aweke mafuta haya juu ya damu kutoka kwenye sadaka ya hatia.
18Kama kwa mafuta yaliyosalia kwamba katika mkono wa kuhani, atayaweka juu ya kichwa cha mtu ambaye atakaswaye, na kuhani atafanya utakaso kwaajili yake mbele za Yahwe.
19Ndipo kuhani atatoa sadaka ya dhambi na kufanya upatanisho kwaajili yake atakaswaye kwa sababu ya kutokuwa safi kwake, na badaye ataua sadaka ya kuchomwa.
20Ndipo kuhani atatoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya nafaka juu ya madhabahu. Kuhani atafanya upatanisho kwaajili ya mtu huyo, na ndipo atakuwa safi.
21Kwa namna hiyo, kama mtu ni masikini na hawezi kumudu matoleo haya, ndipo anaweza kuchukua kondoo mmoja dume kama sadaka ya hatia ya kutikiswa, kufanya upatanisho kwaajili yake mwenyewe, na moja ya kumi ya efa ya unga safi uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, na chombo cha mafuta,
22pamoja na njiwa wawili au kinda mbili za njiwa, ambao anaweza kupata; ndege mmoja atakuwa sadaka ya dhambi na mwingine sadaka ya kuteketezwa.
23Katika siku ya nane lazima awalete kwa kuhani kwaajili ya utakaso, pakuigilia katika hema ya mkutano, mbele ya Yahwe.
24Kuhani atachukua mwana kondoo kwaajili ya sadaka, na atachukua pamoja na kiasi cha mafuta ya mzeituni, na ataviinua juu kama anaviwasilisha kwa Yahwe.
25Atamuua mwana kondoo kwaajili ya sadaka ya hatia, na atachukua baadhi ya ya damu ya sadaka ya hatia na kuiweka juu ya ncha ya sikio la kulia la yule wakutakaswa, juu ya dole gumba la mkono wake wa kulia, na kwenye dole kubwa la mguu, wa kulia.
26Ndipo kuhani atamimina baadhi ya mafuta katika kiganja cha mkono wake wa kushoto,
27na atanyunyiza kwa kidole chake cha kulia baadhi ya mafuta ambayo yako kwenye mkono wa kushoto mara saba mbele za Yahwe.
28Ndipo kuhani ataweka kiasi cha mafuta ambayo yako kwenye mkono wake kwenye ncha ya sikio la yule mtu wa kutakaswa, katika dole gumba lake la mkono wa kulia, na dole kubwa la mguu wa kulia, maeneo yale yale ambayo kaweka damu ya sadaka ya hatia.
29Ataweka mafuta yaliyobaki yaliyo mkononi mwake juu ya yule wakutakaswa, kufanya upatanisho kwaajili yake mbele za Yahwe.
30Lazima atoe sadaka ya njiwa au makinda ya njiwa, yale ambayo mtu ameweza kupata -
31moja kama ya sadaka ya dhambi na nyingine kama sadaka ya kuteketezwa, pamoja na sadaka ya nafaka. Ndipo kuhani atafanya upatanisho kwaajili ya yule ambaye atatakaswa mbele za Yahwe.
32Hii ni sheria kwaajili ya mtu kwake kuna athari za ugonjwa wa ngozi, ambaye hawezi kumudu kiwango cha sadaka kwaajili ya utakaso wake.”
33Yahwe alizungumza na Musa na Haruni, akisema,
34“Wakati mtakuja katika nchi ya Kanaani ambayo nimewapa kama miliki, na kama naweka ukungu unaenea ndani ya nyumba katika nchi ya miliki yenu,
35ndipo yeye ambaye anamiliki nyumba ile lazima aje na kumwambia kuhani. Lazima aseme 'Inaonekana kwangu kuna kitu fulani kama ukungu ndani ya nyumba yangu.'”
36Ndipo kuhani ataamuru kwamba watoe vitu vyote ndani kabla hajaenda ndani kuona uthibitisho wa ukungu, kiasi kwamba hakuna ndani ya nyumba kitakachofanywa najisi. Badaye kuhani lazima aende ndani kuona humo ndani.
37Yeye lazima achunguze ukungu kuona kama umo katika kuta za nyumba, na kuona ikiwa kunaonekana ukijani au wekundu katika bonde za mwonekano wa kuta.
38Kama nyumba inao ukungu, ndipo kuhani atatoka nje ya nyuma na kufunga mlango wa nyumba kwa siku saba.
39Ndipo kuhani atarudi tena katika siku ya saba na kuichunguza kuona kama ukungu umeenea katika kuta za nyumba.
40Kama hivyo, ndipo kuhani ataamuru kwamba wayaondoe mawe ambayo ukungu umepatikana na yatupwe katika sehemu najisi nje ya mji.

Read Mambo ya Walawi 14Mambo ya Walawi 14
Compare Mambo ya Walawi 14:14-40Mambo ya Walawi 14:14-40