Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 13

Mambo ya Walawi 13:6-25

Help us?
Click on verse(s) to share them!
6Naye kuhani atamchunga tena katika siku ya saba ili kuona kama ugonjwa ubepona na haujasambaa zaidi kwenye ngozi. kama haujasambaa, basi, kuhani atamtangaza kuwa yeye ni safi. Ni upele tu. Naye atafua nguo zake, na kisha yeye yu safi.
7Lakini endapo ule upele utakuwa umishasambaa kwenye ngozi baada ya kuwa amejionyesha kwa kuhani kwa ajili kusafishwa kwake, itambidi kujionyesha tena kwa kuhani.
8Naye kuhani atamchunguza ilikuona kama huo upele umsambaa zaidi ndani ya ngozi. Na endapo utakuwa umesambaa, kisha kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni ugonjwa wa kuambukiza.
9Iwapo ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza umo kwa mtu fulani, naye mtu huyo yapasa aletwe kwa kuhan.
10Kuhani atamchunguza ili kuona kama kunauvimbe mweupe katika ngozi yake, endapo malaika zitakuwa zimebadilika kuwa nyeupe, au kumekuwa na nyama mbichi kwenye uvimbe.
11Kama ipo, basi, huo ni ugonjwa sugu wa ngozi, naye kuhani atamtangaza kuwa najisi. Hatamtenga kwa kuwa yeye tayari ni najisi.
12Iwapo huo ugonjwa unajitokeza na kupanuka zaidi kwenye ngozi, na kuifunika ngozi ya mtu kwa ugonjwa tangu kichwani pake hata miguuni, maadamu anajitokeza kwa kuhani,
13naye kuhani atamchunguza ili kuona kama huo ugonjwa umeshaenea mwili wake wote. Ikiwa imetokeo hivyo, kuhani atamtangaza mtu huyo aliye na ugonjwa kuwa ni safi. Ikiwa amebadilika kuwa mweupe, huyo ni safi.
14Lakini ikiwa nyama mbichi imeonekana juu yake, atakuwa najisi.
15Kuhani ataiangalia hiyo nyama mbichi na kumtanga kuwa najisi kwa sababu hiyo nyama mbichi ni najisi. Huo ni ugonjwa wa kuambukiza.
16Lakini endapo hiyo nyama mbichi inageuka kuwa nyeupe tena, naye huyo mtu hana budi kwenda kwa kuhani.
17Kuhani atamchunguza ili kuona kama hiyo nyama imebadilika kuwa nyeupe. Kama imekuwa hivyo naye kuhani atatangaza kwamba mtu huyo kuwa ni safi.
18Mtu anapokuwa na jipu juu yangozi yake na limishapona,
19na mahali pa jipu pamekuwa na uvimbe au doa lenye kung'aa, wekundu unaochanganyikana na weupe, yapasa kuonyeshwa kwa kuhani.
20Naye kuhani atalichunguza ili kuona kama linaonekana limekwenda chini ya ngozi, na kama hizo malaika zimebadilika kuwa nyeupe, kama ni hivyo, kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni ugonjwa wa kuambukiza, endapo utakuwa umezalishwa mahali lilipokuwa jipu hilo.
21Lakini endapo kuhani atakuwa amelichunguza na haoni malaika nyeupe ndani yake, na kwamba iliko chini ya ngozi bali limefifia, kisha kuhani atamtenga kwa siku saba.
22Kama linaenea kwa kupanuka kwenye ngozi, kisha kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni ugonjwa wa kuambukiza.
23Lakini kama hilo doa lenye kung'ara linabaki mahali pake na halijasambaa, basi hilo ni kovu la jipu, naye kuhani atamtangaza kuwa safi.
24Ngozi inapoungua na nyama mbichi ya inamekuwa na wekundu uliochanganyika na weupe au doa jeupe,
25kisha kuhani ataichunguza kuona kama malaika zilizoko kwenye doa hilo zimebadilika na kuwa nyeupe, na kama limeonekana kwenda chini zaidi ya ngozi, kama limekuwa hivyo, basi huo ni ugonjwa wa kuambukiza. Umejitokeza kwenye jeraha la moto, naye kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni ugonjwa wa kuambukiza.

Read Mambo ya Walawi 13Mambo ya Walawi 13
Compare Mambo ya Walawi 13:6-25Mambo ya Walawi 13:6-25