Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 11

Mambo ya Walawi 11:42-47

Help us?
Click on verse(s) to share them!
42Chochote kitambaacho kwa kujivuta juu ya tumbo lake, na chochote kitembeacho kwa miguu yake yote minne, au chochote kilicho na miguu mingi—wanyama wote ambao hutambaa juu ya nchi, hawa msiwale, kwa sababu watakuwa machukizo.
43Msijinajisi wenyewe kwa kiumbe chochote nnajisi kitaambacho; msijinasi wenyewe kwavyo, ili kwamba msije mkachafuliwa navyo.
44Kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu. Nanyi lazima muwe watakatifu, kwa hiyo na iweni watakatifu, kwa sababu Mimi ni mtakatifu. Haiwapasi kujichafua kwa aina yoyote ya kiendacho juu ya nchi.
45Kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh, aliyewaleta ninyi kutoka nchi ya Misri, ili niwe Mungu wenu. Kwa hiyo lazima muwe watakatifu, kwa kuwa Mimi ni mtakatifu.
46Hii ndiyo sheria kuhusu wanyama, ndege, kila kiumbe hai kiendacho majini, na ya kila kiumbe kitambaacho juu ya nchi,
47kwa jili ya kilie kinachopaswa kutofautishwa kati ya kilicho najisi na kilicho safi, na kati ya vitu vilivyokufa na vilivyo hai ambavyo vyaweza kuliwa na vitu vyenye uihai visivyoweza kuliwa.”

Read Mambo ya Walawi 11Mambo ya Walawi 11
Compare Mambo ya Walawi 11:42-47Mambo ya Walawi 11:42-47