Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Mambo ya Walawi - Mambo ya Walawi 11

Mambo ya Walawi 11:3-9

Help us?
Click on verse(s) to share them!
3Mnaweza kula mnyama yeyote aliye na kwato zenye kugawanyika na ambaye pia hucheua.
4Hata hivyo, kuna baadhi ya wanyama ambao ama hawacheui au hana kwato zilizogawanyika, nanyi msiwale hao, wanyama kama ngamia, kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato zilizogawanyika. Kwa hiyo ngamia ni najisi kwenu.
5Pimbi pia: kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato zilizogawanyika mara mbili, huyo pia ni najisi kwenu.
6Na sungura pia: kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato zilizogawanyika mara mbili, huyu naye ni najisi kwenu.
7Na nguruwe pia: ingawaje yeye anazo kwato zilizogawanyika lakini hacheui, kwa hiyo yeye ni najisi kwenu.
8Msile aina yoyote ya nyama yao, wala msiiguse mizoga yao. Hao ni najisi kwenu.
9Nao wanyama waishio majini mnaoweza kuwala ni wale wote walio na mapezi na magamba, iwe waliomo baharini au mitoni.

Read Mambo ya Walawi 11Mambo ya Walawi 11
Compare Mambo ya Walawi 11:3-9Mambo ya Walawi 11:3-9