Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 4

Luka 4:4-18

Help us?
Click on verse(s) to share them!
4Yesu akamjibu, “Imeandikwa; 'mtu hataishi kwa mkate pekee.”
5Kisha Ibilisi alimwongoza juu kwenye kilele cha mlima, na akamwonyesha falme zote za dunia kwa muda mfupi.
6Ibilisi akamwambia, “Nitakupa mamlaka ya kutawala falme hizi zote pamoja na fahari zake. Naweza kufanya hivyo kwa sababu vyote vimekabidhiwa kwangu nivitawale, na ninaweza kumpa yeyote nitakaye kumpa.
7Kwahiyo, kama utaniinamia na kuniabudu, vitu hivi vyote vitakuwa vyako.”
8Lakini Yesu alijibu na kumwambia, “Imeandikwa, “lazima umwabudu Bwana Mungu wako, na lazima umtumikie Yeye peke yake.”
9Baadaye Ibilisi alimwongoza Yesu hadi Yerusalemu na kumweka sehemu ya juu kabisa ya jengo la hekalu na kumwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini kutoka hapa.
10Kwa sababu imeandikwa, “Atawaagiza malaika zake wakutunze na kukulinda,
11na watakuinua juu mikononi mwao ili kwamba usiumize miguu yako juu ya jiwe.”
12Yesu akijibu alimwambia, “Imenenwa, “usimjaribu Bwana Mungu wako.”
13Ibilisi alipomaliza kumjaribu Yesu, alienda zake na kumwacha hadi wakati mwingine.
14Kisha Yesu alirudi Galilaya kwa nguvu za Roho, na habari kumhusu yeye zikaenea na kusambaa katika mikoa jirani yote.
15Alifundisha katika masinagogi yao, na kila mmoja alimsifu.
16Siku moja alikwenda Nazareti, mji ambao alilelewa na kukulia. Kama ilivyokuwa desturi yake aliingia kwenye sinagogi siku ya sabato, na alisimama kusoma maandiko.
17Alikabidhiwa gombo la nabii Isaya, hivyo, alilifungua gombo na akatafuta sehemu iliyoandikwa,
18“Roho wa Bwana yuu juu yangu, kwa sababu alinitia mafuta kuhubiri habari njema kwa maskini. Amenituma kutangaza uhuru kwa wafungwa, na kuwafanya wasioona waweze kuona tena. Kuwaweka huru wale wanaogandamizwa,

Read Luka 4Luka 4
Compare Luka 4:4-18Luka 4:4-18