Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 2

Luka 2:40-52

Help us?
Click on verse(s) to share them!
40Mtoto alikua, na akawa na nguvu, akiongezeka katika hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.
41Wazazi wake kila mwaka walikwenda Yerusalemu kwaajili ya sikukuu ya Pasaka.
42Alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, walikwenda tena wakati mwafaka kidesturi kwa ajili ya sikukuu.
43Baada ya kubaki siku zote kwa ajili ya sikukuu, walianza kurudi nyumbani. Lakini mvulana Yesu alibaki nyuma mle Yerusalemu na wazazi wake hawakujua hili.
44Walidhani kwamba yumo kwenye kundi walilokuwa wakisafiri nalo, hivyo walisafiri safari ya siku. Ndipo wakaanza kumtafuta miongoni wa ndugu na marafiki zao.
45Waliposhindwa kumpata, walirudi Yerusalemu na wakaanza kumtafuta humo.
46Ikatokea kwamba baada ya siku tatu, wakampata hekaluni, akiwa ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali.
47Wote waliomsikia walishangazwa na ufahamu wake na majibu yake.
48Walipomwona, walistaajabu. Mama yake akamwambia, “Mwanangu, kwa nini umetutendea hivi? Sikiliza, baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa wasiwasi mkubwa.”
49Akawaambia, “Kwa nini mmekuwa mkinitafuta? Hamkujua kwamba lazima niwe kwenye nyumba ya Baba yangu?
50Lakini hawakuelewa nini alichomaanisha kwa maneno hayo.
51Ndipo akaenda pamoja nao mpaka nyumbani Nazareti na alikuwa mtii kwao. Mama yake alihifadhi mambo yote moyoni mwake.
52Lakini Yesu aliendelea kukua katika hekima na kimo, na akazidi kupendwa na Mungu na watu.

Read Luka 2Luka 2
Compare Luka 2:40-52Luka 2:40-52