Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Luka - Luka 20

Luka 20:13-18

Help us?
Click on verse(s) to share them!
13Hivyo bwana wa shamba akasema, 'Nitafanya nini? Nitamtuma mwanangu mpendwa. Labda watamheshimu.'
14Lakini wakulima wa mzabibu walipomwona, walijadili wao kwa wao wakisema, `Huyu ndiye mrithi. Tumuue, ili urithi wake uwe wetu.'
15Wakamtoa nje ya shamba la mizabibu na kumuua. Je bwana shamba atawafanya nini?
16Atakuja kuwaangamiza wakulima wa mzabibu, na atawapa shamba hilo wengine”. 'Nao waliposikia hayo, wakasema, 'Mungu amekataa'
17Lakini Yesu akawatazama, akasema, “Je andiko hili lina maana gani? 'Jiwe walilolikataa wajenzi, limekuwa jiwe la pembeni'?
18Kila mtu aangukaye juu ya jiwe hilo, atavunjika vipande vipande. Lakini yule ambaye litamwangukia, litamponda.'

Read Luka 20Luka 20
Compare Luka 20:13-18Luka 20:13-18